MAPIGANO baina ya Kabila la Wasonjo na
kabila la Wamasai wa Loita kutoka nchini Kenya yanayoendelea katika Kata
ya Samunge wilayani Ngorongoro mkoani Arusha yameonesha kiwango cha
ukatili binadamu anachoweza kufikia, baada ya kupatikana kwa mifupa ya
mtoto iliyewambwa mtini.
Taarifa kutoka eneo la mapigano linasema
kwamba mtoto huyo ambaye mifupa yake ilikutwa alifahamika kwa jina la
Njibula Philemon(14) kutoka katika eneo la Kis
angiro na inasemekana
aliuawa na kisha kuwambwa juu ya mti kiasi cha miezi mitatu iliyopita.
Tukio hilo ni moja ya matukio mawili ya
mauaji katika mapigano yanayoendelea. Akiongelea tukio hilo Mwenyekiti
wa kijiji cha Kisangiro , Timothy Thomas alidai kuwa mtoto huyo alipotea
katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika shughuli za ufugaji yeye,
ndugu yake na baba yake mzazi.
Timothy alidai kuwa wakati wakiwa katika
shughuli zao za ufugaji baba yake mzazi alikwenda kutafuta chakula
lakini aliporudi hakumuona tena hadi alipopatikana akiwa amewambwa
kwenye mti mkubwa huku nyama zake zote zikiwa chini na kubaki mifupa.
“Mara zote tunapoona tatizo huwa tunatoa
taarifa kwa Polisi lakini wakati mwingine wanadai kuwa sisi ni waongo
hakuna matukio kama hayo hivyo basi tuliamua kuzika mifupa tuu ya kijana
wetu pamoja na baadhi ya nyama za mwili wake, “ aliongeza Timothy.
Katika tukio jingine Kaimu Mwenyekiti wa
Kijiji hicho cha Samunge Jonas Gilobei alisema mauaji ya mtoto wa pili
Kelvin Ndambiseya (8) yalifanyika Mei 10 mwaka huu eneo la mlima
Ngaremishani Kitongoji cha Mijuti.
Alidai wakati kundi la Wamasai
wanawavamia wafugaji hao waliokuwa wakubwa walikimbia kwa kuwa hawakuwa
na silaha lakini mtoto huyo aliamua kujificha kwenye kundi kubwa la
ng’ombe.
Aliendelea kufafanua kuwa wakati akiwa amejificha kwenye kundi hilo Wamasai waliweza kumuona mtoto yule na kumpiga risasi.
Alidai kuwa mara baada ya mtoto huyo
kuuliwa katika mgogoro huo, wafugaji wengine waliokimbia katika eneo
hilo walikuja kutoa taarifa kwa wanakijiji wengine ambao walilazimika
kwenda kwenye eneo la tukio ambapo wale waliofika kwanza waliweza kuona
mwili wa kijana huyo akiwa amekufa pamoja na mbwa wake.
Pia alisema kuwa mara baada ya hapo
walijipanga na kuingia msituni kwa ajili ya kutafuta mwili huo ambapo
hakupatikana hali ambayo inaongeza majonzi katika eneo hilo siku hadi
siku.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha Liberatus Sabas alidai kuwa mpaka sasa ana taarifa juu ya
kupotea kwa mtoto yatima Kelvin Nambiseya lakini bado hana taarifa juu
ya kifo chake wala mtoto aliyewambwa juu ya mti kwa miezi 3.
0 comments:
Post a Comment