Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisko Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat lebulu, na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.
Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regin
a Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward.
Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema
Daud, Beata Cornel na Debora Joachim
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo , ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.
Wakati huo huo jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.
Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimesema kuwa wakati wa tukio hilo walifika watu wawili wakiwa na pikipiki, na kutoa kitu kilichorushwa wakati wa kukatwa utepe wa uzinduzi wa kanisa hilo. Chanzo http://mrokim.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment