BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Millionaire  Ads

MWANAMKE NCHINI BANGLADESH ANUSURIKA KIFO KWA SIKU 17 BAADA YA JENGO LA GHOROFA 8 KUPOROMOKA.

Mwanamke wa Bangladesh anusurika baada ya siku kumi na sab
a.
WAOKOAJI nchini Bangladesh wamemuokoa mwanamke mmoja kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka yapata siku 17 zilizopita. 

Zaidi ya watu 1000 wamethibitishwa kufariki wakati jengo hilo la orofa 8 lilipoporomoka nje kidogo ya mji mkuu Dhaka.

Waokoaji hao wametaja hilo kama miujiza, Ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili tangu jengo hilo la orofa nane kuporomoka, walikuwa tayari wameshaanza kukata tamaa ya kumpata mtu mwengine yoyote hai.

Lakini wanajeshi walipokuwa wanazoa zoa vifusi katika ghorofa ya chini walisikia sauti ikiita. Walitumia vifaa vyao maalum ambavyo vilionyesha dalili za uhai chini ya vifusi.

Mwanamke huyo aliitana akitaja jina lake kama Reshma. Baada ya juhudi za pamoja waokoaji pamoja na wanajeshi walifanikiwa kumtoa mwanamke huyo alikonaswa na kumkimbiza hospitalini.
waokoaji walianza kupoteza matumaini
Ajali hiyo ya Bangladesh imesababisha mataifa mengine hasa ya magharibi kama vile Uingereza kutilia shaka bidhaa za kutoka nchini Bangladesh kwa namna zinavyotengenezwa na uwezekano wa kunyanyaswa wafanyikazi.
Chanzo: bbc swahili.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment
Millionaire  Ads