Waombolezaji wakitoa mwili wa marehemu Zulu
kuiingiza kwenye gari
|
MWILI wa Ofisa Habari Mkuu wa Bunge, Ernest Zulu (56)
aliyefariki Mei 23 mwaka huu nchini Malaysia alikokuwa masomoni, umewasili
nchini majira ya saa 1.30 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.
Majira ya mchana mke wake Theresia Zulu na watoto wake walifika
kumtambua marehemu na kisha kundi la waombolezaji lilimsindikiza marehemu
katika gari ili kuanza safari yake ya mwisho kabla ya kwenda
kupu
mzika milele kijiji kwao ndilima, Songea vijijini.
Kwa wakazi wa dare s salaam Zulu ataagwa kesho nyumbani kwake
Ubungo Kibangu.
Baadhi ya watu waliokuwapo mchana wa leo uwanja wa ndege
kuupokea mwili wa Zulu ni Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na waumini wa
Kituo cha Maombezi cha Marian Ubungo, wakiongozwa na Padri Felician Nkwera.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu ambaye hakuwa
tayari kutaja jina gazetini , Zulu alikutwa damu zikimtoka sehemu ya
kichwa na kuegama mezani akiwa ameshika msalaba na picha ya Bikira Maria
vilivyokuwa chumbani.
Awali, taarifa ya Katibu huyo kuhusu kifo hicho, iliyotolewa na
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge, Dodoma
ilieleza kuwa Zulu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa kwa muda mrefu.
Zulu aliyeacha mjane na watoto wanne, Philomena, Maria
Emmaculate, Felistas na Augustina, alikuwa nchini Malaysia, akisoma
Shahada ya kwanza ya Mawasiliano na Usimamizi wa Vyombo vya Habari katika Chuo
Kikuu cha Taylor tangu Julai 2010, na alitarajiwa kumaliza masomo yake Julai,
mwaka huu.
Alizaliwa Julai 10 mwaka 1957 huko Songea.
Alipata elimu ya
msingi na sekondari Songea kabla ya kusomea uandishi wa habari katika Chuo cha
Uandishi wa Habari (TSJ) (sasa SJMC-UDSM) jijini Dar es Salaam.
Aliwahi kufanyakazi katika Shirika la Utangazaji la Tanzania (RTD)
sasa TBC Taifa mwaka 1976 kama Mwandishi wa Habari Msaidizi na hatimaye
kupandishwa cheo kuwa Mwandishi wa Habari kabla ya kuhamia Shirika la Magazeti
la Chama (Uhuru na Mzalendo) kama Mwandishi Mwandamizi mwaka 1985.
Mwaka 1986 hadi 1987 alipata fursa ya kusomea masomo ya Uandishi
wa Habari ya Kimataifa huko nchini Urusi. Mwaka 1991 aliajiriwa kama Mhariri
Msaidizi katika gazeti la The Express kabla ya kujiunga na Sauti ya Ujerumani
ambapo alifanya kazi kama Mwandishi Mwandamizi kuanzia mwaka 1995.
0 comments:
Post a Comment