KIJANA mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja anayedaiwa
ni mzoefu wa wizi kwa kutumia usa
firi wa pikipiki ‘bodaboda’, ameuawa baada ya
kumliza mwanamke aliyetambulika kwa jina la Jusmini.
Tukio hilo lilitokea
mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, saa tatu usiku ambapo
inadaiwa mwanamke huyo alikuwa akikatiza mitaa hiyo huku akiwa ameweka mkoba
wake kwapani.
Ikadaiwa mwanamke huyo akiwa
eneo hilo huku akiamini yuko salama, ilitokea bodaboda kwa nyuma ikiwa imebeba
abiria na ghafla alishangaa anakwapuliwa mkoba wake.
“Unajua yule mama alikuwa
akitembea kwa kujiamini lakini inavyoonekana wale jamaa ambao ndiyo zao
kuwaibia watu walikuwa wamemlia ‘timing’ tangu aliposhuka kwenye daladala.
“Tuliposikia makelele ya
mwizi, tulimfuata mama huyo na tulipomuuliza akatuambia ameibiwa mkoba wake
huku akituonesha vijana hao ambao muda huo walikuwa wakikimbia,” kilieleza
chanzo hicho kilichoshuhudia tukio zima.
Ikaelezwa kuwa, kufuatia
maelezo ya mwanamke huyo, baadhi ya watu wenye hasira kali wengine wakiwa
kwenye pikipiki waliamua kuwakimbiza wezi hao ambapo mmoja alishuka na kukimbia
kivyake huku mwenye bodaboda akizuiwa kwenye geti kuu ya kutokea magari.
“Alipozuiwa akaona imeshakua
soo, akashuka na kuitelekeza pikipiki yake kisha akataka kudandia gari nyingine
lakini watu wakafanikiwa kumkamata kwenye mataa ya Mwenge ambapo magari
yalisimama, jamaa alishushiwa kichapo hadi akauawa,” kiliendelea kupasha chanzo
hicho.
Baada ya kijana huyo kuuawa,
polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wake.
Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela (pichani)alipoulizwa kuhusiana na tukio
hilo alisema taarifa za kifo cha kijana huyo hazijafika mezani kwake lakini
akasema anaendelea kufuatilia.
0 comments:
Post a Comment