Mbunge wa Arusha Mjini Chadema, Godbless Lema.
Arusha,Tanzania
SIKU moja baada ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kusema
kwamba, ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ambayo Mbunge wa Arusha Mjini
(Chadema) Godbless Lema alidai kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Magesa Mulongo si ya kweli,Mbunge huyo huwenda akaongezea mashtaka.
Katika ujumbe huo Mbunge huyo alidai kwamba Mulongo alimtumia ujumbe
mufupi uliosomeka kwamba, "Umeruka kihunzi cha kwanza,nitakuonyesha mim
i
ni Serikali, ulikojificha nitakupata na kukupa kesi ninayotaka mimi,
"ilisema sehemu ya ujumbe huo.
Wakati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akitangaza
kwamba ujumbe huo haukutumwa na mtumiaji wa simu za makampuni ya simu
Tanzania, bali ilitumwa na makampuni za nje ya nchi, duru za ndani ya
jeshi la Polisi zinadai kwamba, huenda Mbunge huyo akabadilishiwa
mashtaka ama kuongezewa mashtaka mengine, kutokana na taarifa
zilizotangazwa na jeshi hilo kutoka Vodacom kwamba ujumbe wa maandishi
ya vitisho aliyotumiwa Mbunge huyo na mtu aliyedai kwamba ni Mkuu wa
Mkoa huo si za kweli na kuongeza kasi katika shtaka la uchochozi.
Kamanda Sabas alisema, "Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi
kufuatia tuhuma hizo ambazo Mkuu wa Mkoa Mulongo kukanusha ujumbe huo
uliodaiwa kutumwa kupitia namba ya simu ya Mulongo kwenda kwa Lema".
Katika kesi inayomkabili Mbunge huyo itakayosikilizwa tena Mei 29 mwaka
ni pamoja na shitaka la kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu
alipokwenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.
Haki
hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa
kupiganiwa.
Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa "Tumemtafuta mkuu wa
mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na
kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.
CHANZO http://www.habarimpya.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment