Baadhi ya mashamba ya wananchi eneo la Rongai, wilayani Rombo ambayo mara kadhaa huvamiwa na Tembo waharibifu.
Pichani
ni baadhi ya majengo ya Shule ya Msingi Rongai, wilayani Rombo. Shule
hii ni miongoni mwa maeneo yan
ayoathiriwa na uvamizi wa Tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.
ayoathiriwa na uvamizi wa Tembo waharibifu ambao huathiri taaluma shuleni hapo.
Na Thehabari.com, Rombo
Halmashauri
ya Wilaya ya Rombo imeanza mipango ya kutumia ufugaji wa nyuki kukabiliana na
tembo waharibifu ambao mara kadhaa huvamia baadhi ya makazi ya wananchi maeneo
mbalimbali ya wilaya hiyo na kufanya uharibifu wa mazao pamoja na kuua au
kujeruhi wakazi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani Rombo, Mkurugenzi Mtendaji
wa halmashauri hiyo, Judethadeus Mboya alisema tayari halmashauri hiyo
imetengeneza mizinga ya nyuki ambayo imesambazwa maeneo kadhaa ili kukabiliana
na tembo waharibifu eneo hilo.
“Unajua
nimetembea mbuga mbili za Kenya ikiwemo Tsavo ambazo tumepakana nazo eneo hili
sehemu ambayo tembo hutokea huko na kuvamia maeneo yetu, sehemu hizi wao
wamedhibiti uvamizi wa tembo…wamefuga nyuki wengi sana na maeneo mengine
wametumia hadi teknolojia kuwazuia tembo kuvamia makazi ya raia hivyo hawapati
madhara kama yetu,” alisema Mboya akifanya mazungumzo na gazeti hili ofisini.
Amesema
kwa sasa tayari wametengeneza mizinga 50 ya nyuki na kuifunga ukanda wa chini
wa vijiji kama Chala, Ibukoni, Ngoyoni na maeneo mengine ambayo tembo huyatumia
kama njia kipindi cha uvamizi na kwa sasa mizinga mingine 100 ya nyuki
inaandaliwa kuenezwa maeneo mengine kukabiliana na tembo hao hatari.
Amesema
viongozi wa halmashauri hiyo pia wametoa elimu kwa wanakijiji maeneo husika ya
kuhamasisha uvugaji nyuki katika vikundi ikiwa ni jitihada za kukabiliana na
tembo hao waharibifu ambao idadi kubwa hutokea nchi jirani ya Kenya na kufanya
uharibifu pamoja na kutishia maisha ya wanavijiji upande wa Tanzania.
Aidha
kiongozi huyo alisema tembo hao mbali na kufanya uhalibifu mkubwa wa mazao ya
wanavijijini kipindi cha uvamizi wakati mwingine wamekuwa wakiuwa raia jambo
ambalo ni hatari zaidi kiusalama.
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi umebaini uvamizi wa wanyama hao umekuwa kero kwa maeneo
mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo, kiasi ambacho unatishia shughuli za
maendeleo ya wananchi kama kilimo pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.
Akizungumzia
hali ya uvamizi wa tembo na athari za elimu, Mwalimu wa Taaluma Shule ya
Sekondari Tanya, Shuma Himidiel alisema miezi ambayo tembo huanza kufanya
uvamizi huingilia ratiba za masomo na mara kadhaa kusimama kutokana na hofu ya
wanafunzi na usalama wao hasa wanapotoka na kuja shuleni.
“Kimsingi
wanyama hawa wanapoanza usumbufu kijiji kizima huwa na heka heka na wakati
mwingine hata wanafunzi wanashindwa kuja shule kuhofia maisha yao…hata wazazi
huwazuia watoto wao kutoka hadi hali ya hatari inaporejea kuwa ya kawaida.
Akifafanua
zaidi mwalimu Himidiel alisema mara ya mwisho tembo kufanya uvamizi katika
Kijiji cha Tanya waliua mtu mmoja walipokuwa wakidhibitiwa na askari wa
wanyamapori eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment