MWANANCHI.
KAMA kuna eneo ambalo Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa ni
udhibiti wa usafiri wa pikipiki, maarufu kama Bodaboda. Udhaifu huo
umetoa mwanya kwa waendesha Bodaboda kuweka kando sheria za usalama
barabarani na kufanya usafiri huo kuwa janga la kita
ifa kutokana na kusababisha ajali zinazoua maelfu ya watu kila mwaka, huku maelfu ya majeruhi wakiwa wamepoteza viungo muhimu katika miili yao.
ifa kutokana na kusababisha ajali zinazoua maelfu ya watu kila mwaka, huku maelfu ya majeruhi wakiwa wamepoteza viungo muhimu katika miili yao.
Licha ya Jiji la Dar es Salaam kuwa machinjio
makuu ya wahanga wa ajali hizo, tatizo hilo limeikumba Tanzania Bara
kuanzia kata hadi makao makuu ya mikoa. Waendesha Bodaboda na abiria wao
wanakufa ovyo kila siku katika ajali. Serikali imebaki kuwa mtazamaji
na kujivua jukumu la kuhakikisha kwamba inalinda maisha ya raia wake.
Taarifa za Jeshi la Polisi zimethibitisha kuwapo
watu wengi wanaopoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya katika ajali
hizo, hivyo kupoteza rasilimali kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu. Kwa
mfano, takwimu za ajali hizo mkoani Dar es Salaam zinatisha.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema watu 1,875 walikufa jijini katika kipindi cha 2011/12 kutokana na ajali za barabarani, ikiwa ni wastani wa vifo vya watu watatu kila siku.
Takwimu za 2012/13 bado zinakusanywa, lakini jeshi hilo linasema idadi ya watu waliokufa nchi nzima tangu mwanzoni mwa mwaka huu ni kubwa mno ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita. Madaktari na wauguzi wamesema wameelemewa na idadi kubwa ya majeruhi hao.
Wengi wamepoteza viungo muhimu, hivyo wamebaki kuwa tegemezi.
Wamekata tamaa.

Ni wimbi hilo la majeruhi ambalo limezilazimisha
hospitali nyingi nchini, zikiwamo Bugando, Tumbi na Muhimbili kutenga
vitengo maalumu kwa ajili ya waathirika wa ajali za Bodaboda. Katika
Kitengo cha Mifupa Muhimbili, wauguzi walilalamika hivi karibuni kwamba
wanaumwa migongo kutokana na kuhudumia majeruhi wengi wa ajali hizo
ambao wanalala chini kutokana na uhaba wa vitanda.
Hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu, kwani
asilimia kubwa ya waathirika wa ajali hizo ni vijana ambao ndiyo ‘taifa
la kesho’. Maana yake ni kwamba taifa la kesho litakuwa la watu
wasiojiweza, wasiokuwa na mikono wala miguu. Tunapoteza rasilimali kubwa
ya taifa letu kila kukicha na Serikali imebakia tu kuwa mtazamaji.
Udhaifu wa Serikali umezalisha madereva wa
Bodaboda ambao wanaweza kulinganishwa na vichaa waliosheheni mapanga na
majambia kisha kumwagwa katikati ya umati mkubwa wa watu. Hawana elimu,
leseni wala bima, hawajui sheria za usalama barabarani, wanashindia
viroba na misokoto ya bangi. Hawalipi kodi. Hawana cha kupoteza.
Lazima tukubali kwamba usafiri wa Bodaboda ni
jambo la kudumu. Kuupiga marufuku ni kukaribisha maafa mapya ya vijana
hao kurudi mitaani na kunyonga watu.
Serikali inachopaswa kufanya ni kuanzisha kitengo maalumu ndani ya Kikosi cha Usalama Barabarani kusimamia usafiri wa miguu miwili na mitatu, yaani Bodaboda na Bajaji.
Waendesha Bodaboda na Bajaji kuanzia ngazi za wilaya wapewe mafunzo, wasajiriwe na wavae vazi maalumu, huku Bodaboda na abiria wao wakilazimika kisheria kuvaa kofia ngumu.

Nchi nyingi barani Afrika, zikiwamo Uganda na
Rwanda zimefanikiwa kuuratibu usafiri huo na kupunguza ajali. Ni fursa
nzuri kwa Serikali yetu kuchukua hatua sasa, siyo kesho.
0 comments:
Post a Comment