SERIKALI ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na
Makamu wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi
CD zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO, MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH
ILUNGA.
Agizo hilo lilitolewa na
OCD wa zamani Murtad MKADAM ambae kwa sasa yupo ofisi kuu ya
polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim
Seif.
Alisema cd hizo za kiislam
ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha ucho
chezi
baina ya dini ya ukiristo na uislam.
SHEIKH
ILUNGA.
OCD alibainisha kuwa mpaka
sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha na kuuza cd hizo na
kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani
serikali ina mkono mrefu.
Akijibu baadhi ya maswali
aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya
biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala
sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani
katika nchi.


0 comments:
Post a Comment