KWA mara ya kwanza nyota wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya
kueleza sababu za kwanini ni kiwembe ?.
Akifunguka katika mahojiano
maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye
ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za
kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO
Kabla ya yote, staa huyo
alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake
wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na
msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.
KWA NINI ANAPENDA
KUBADIL
ISHA WANAWAKE ?.
Diamond: Mimi ni binadamu
kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na
kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu
nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA
KIPINDI CHA MIAKA MITATU ?.
Diamond:
Nikiwa na mtu
nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na
wanawake wenye majina.
Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu
lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi
sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama
naonekana msumbufu.
KWA NINI MASTAA, TENA
MARAFIKI ?.
Diamond: Huwa sitoki, nakuwa
nyumbani tu, nakaa na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) nampikia. Nikitoka
nakwenda kwenye shoo au studio. Huko ndiko nakutana nao (mastaa wa kike).
ALIMPATAJE JOKATE (MWEGELO) ?
Diamond: Alikuwa anazindua
nguo zake (Kidoti) akaniomba nikapite nazo kwenye onesho la mavazi, nikapita
nazo jukwaani. Baada ya hapo na mimi nilimuomba nifanye naye video ya wimbo
wangu (Mawazo), ndiyo ikatokea kama hivyo.
NINI KILIMVUTIA KWA PENNY ?.
Diamond: Kwanza mimi
nilimjua Penny kabla ya Wema (Sepetu), alikuwa mshikaji wangu. Ni mwanamke
mzuri, wa kileo, ana akili adabu na heshima. Anampenda mama yangu na familia
yangu ‘coz’ na mimi nampenda mama yangu (sifa ambazo kwa mujibu wake Wema
alizikosa).
KWA NINI ALIMREKODI WEMA ?.
Diamond: Kila binadamu
anajiona yupo sawa na anaonewa. Sipendi kuongea, nitazungumza vibaya. Mapenzi
yanaumiza na mimi naumia pia lakini watu wanadhani mimi ndiye muumizaji. Unamwambia
mtu kwa nini una mwanaume mwingine.
Anakuzuga sijui ni pedeshee
anampa pesa. Mara unamwona na mwanaume mwingine. Mimi siyo maskini lakini sasa
mara unamwona na brazameni mwingine ‘then’ washkaji wanakwambia. Wewe
unajifanya kuziba masikio mara unasikia ana mwanaume mwingine. Lakini ikafika
wakati nikajikuta naumia sana kwenye mapenzi.
Kama ukisikiliza ule wimbo
wa Kesho ni kweli kabisa. Mimi nikakaa pembeni hadi nilipompata huyu wa sasa
(Penny).
Nakumbuka (Wema) alinipigia
simu akadai mimi ndiye nasema anataka turudiane. Nilikuwa kwenye gari,
nikamuuliza anataka nini?
Wakati huo nilishafika
nyumbani kwa baby wangu. Nikamwonesha ona sasa, anasema mimi ndiyo nataka
nirudiane naye, anatangazia watu hadi saluni kuwa nataka kurudiana naye na
kujidai kwenye vyombo vya habari kuwa ananipenda. Kumbe ana wengine (ving’asti)
kama ishirini anawahonga (mistari ya wimbo wake wa Nataka Kulewa).
Nilimpa baby wangu
akamwambia kistaarabu tuache tulale. Sasa kuna mtu wetu wa karibu ndiye
aliyehusika kusambaza ile sauti.
SEMA UKWELI, ULILALA NA
UWOYA ?.
Diamond: (kicheko)
Ningeanzia wapi? Unajua mimi ni simba kwa hiyo nikionekana na swala inajulikana
lazima nimle hata kama tumeenda sehemu tu kuzungumza ishu za kazi.
KWA NINI WANAWAKE AU ENZI
ZILE HAKUWA NA ‘CHANSI’ SASA AMEPATA ?.
Diamond: Ukimuelimisha
mwanamke mmoja umeelimisha ulimwengu mzima. Nawapenda sana, wanajaa tele kwenye
shoo zangu. Kilichotokea kwa Wema ilibidi tu sikuwa na jinsi.
ANATAKA MWANAMKE WA AINA
GANI ?.
Diamond: Ukimuuliza mwanamke
aliyewahi kuwa na mimi atakwambia najua mapenzi, najua kupetipeti, najua
kubembeleza, najua kujifanya mjinga. Narudia tena, awe mzuri, wa kileo, mwenye
akili, anayejiheshimu, ampende mama yangu kama mimi ninavyompenda mama yangu.
KWA NINI KIWEMBE ?.
Uchunguzi uliofanywa
ulibaini kuwa chanzo cha staa huyo aliyetokea Tandale, Dar kuitwa kiwembe ni
kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake kama nguo.
Baadhi ya aliowahi
kuripotiwa akidaiwa kutoka nao ni Rehema Fabian (Miss Kiswahili 2009),
Jacqueline Wolper (msanii wa filamu), Upendo Moshi ‘Pendo’ (Mshiriki wa Maisha
Plus) na Natasha (Video Queen wa Bongo Fleva).
Wengine ni Wema (mwigizaji),
Jokate (mwigizaji), Aunt Ezekiel (mwigizaji), Najma (msanii wa Bongo Fleva),
Penny (mtangazaji DTV), Irene Uwoya (mwigizaji) na wengineo.

0 comments:
Post a Comment