BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TAARIFA ZA LEO KUTOKA MTWARA KUHUSU VURUGU ZA JANA

clip_image001Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza.
Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigw mfululizo.
 Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
 Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)

 Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani  maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume  na kumkamata..
RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.
Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: