MKUU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO (MSJ) AUGUSTINE NONGWE AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MDAHALO WA KUJADILI SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UKUMBI WA JKT NANE NANE UWANJA WA KIMATAIFA WA MAONYESHO YA WAKULIMA WA MWL JULIUS NYERE KANDA YA MASHARIKI MOROGORO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MAANDAMANO, KUTOKA KUSHOTO NI MRATIBU WA MAFUNZO CHUO HICHO JOHN KIDASI NA (KATIKATI) NI MHARIRI MKUU WA KITUO CHA SUATV MKOANI MOROGORO BUJAGA KADAGO. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPO.COM
MKUFUNZI KATIKA CHUO HICHO CHA MSJ EFRASIA MATHIAS AKIWALISHA MADA KATIKA MADA KATIKA MDAHALO HUO.
MWANAFUNZI WA MWAKA WA PILI MAWASILIANO YA UMMA CHUO KIKUU CHA WAISLAM MOROGORO (MUM) AMOUR SALIM ABDI NAYE AKIWASILISHA MADA KATIKA MDAHALO HUO.
RAIS WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO (MSJ) GODFREI MARUSU KULIA AKIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VYA JODARN COLLAGE MOROGORO, WAISLAM MOROGORO, ROYAL COLLAGE TANZANIA AMBAO WALIWAONGOZA WANAFUNZI WA VYUO HIYO WAKATI WA MDAHARO WA KUJADILI MASWALA YA UHURU WA VYOMBO VYAA HABARI KATIKA UKUMBI WA JKT NANE NANE ULIOPO NDANI YA UWANJA WA KIMATAIFA WA MAONYESHO YA WAKULIMA KANDA YA MASHARI WA MWL JULIUS NYERE
RE MOROGORO.WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA WAISLMA MOROGORO (MUM)
WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA BAHARI MOROGORO (MSJ).
SEHEMU YA WANAFUNZI WA CHUO CHA ROYAL COLLAGE OF TANZANIA KUTOKA DAR ES SALAAM WAKIFUATILIA MATUKIO YALIYOKUWA YAKIENDELEA KATIKA UKUMBI HUO.
SEHEMU YA WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI WAKIFUTIALIA MATUKIO YALIYOKUWA YAKIENDELEA KATIKA MDAHARO WA KUJADILI MASUALA YA UANDISHI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
MHARIRI MKUU WA KITUO CHA LUNINGA CHA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA) SUATV MKOANI MOROGORO BUJAGA KADAGO KULIA AKIPOKEA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA CHUO CHA WAANDISHI WA HABARI MOROGORO ( MSJ) KATIKA UKUMBI WA JKT NANE NANE YALIYOANZIA CHUONI KWAO WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO.
HATA MKITUTISHIA BUNDUKI ILA UKWELI TUTASEMA NDIVYO BANGO LINAVYOSEMA KWA WANAFUNZI HAO MARA BAADA YA MAANDAMANO YAO KUPOKEWA NA MHARI MKUU WA KITUO CHA SUATV MKOANI MOROGORO BUJAGA KADAGO (HAYUPO PICHANI) KATIKA UKUMBI WA JKT NANE NANE.
WANAFUNZU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI MOROGORO (MSJ) WAKIWA NA MABANGO YENYE UJUMBE MBALIMBALI UKIWE ULE WA "tunakosa uhuru na usalama kwa sababu ya ukweli" WAKATI WA MAADHIMISI HAYO YA SIKU UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI MOROGORO.
HAWA HAWAKUWA NA HAJA YA KUBEBA MABANGO HUKU WAKITEMBEA MDOGO MDOGO.
USALAMA wa waandishi wa habari nchini umetajwa kuwa shakani, hasa
kutokana na kukithiri kwa matukio ya wanataaluma hao kunyanyaswa,
kuteswa na kunyimwa haki zao.
Wadau mbalimbali wa masuala ya habari na
haki za binadamu walitoa tathimini hiyo jana, wakati wa maadhimisho ya
siku ya vyombo vya habari duniani, ambayo kitaifa yamefanyika jijini
Arusha.
Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
Akitoa salamu zake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Richard Sezibera alisema waandishi wa habari wana wajibu wa kuhubiri amani, licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.
“Kwanza natoa pole kwa waliopoteza maisha, walioteswa na wahanga wengine katika tasnia yenu, lakini bado mna wajibu wa kuwekeza katika kuhubiri amani bila kuchoka,” alisema.
Richard aliwataka waandishi habari kuchapa kazi na kukosoa pale inapobidi, kwani anaamini kuwa siku za giza na utawala wa kimabavu zimekwishapita kutokana na mabadiliko ya upashanaji habari duniani.
Alisisitiza kuwa pamoja na kudai uhuru zaidi wa kupata na kutoa habari, vyombo vya habari na waandishi wa habari wanatakiwa kutenda kwa mambo yote, yaani uhuru na uwajibikaji.
"Msisubiri vyombo vya habari vya nje kuyasema mazuri au mabaya yetu, nawaomba ninyi muandike mambo mazuri katika nchi zetu,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye historia yake inaonesha amekuwa na misuguano na waandishi wa habari, jana alijirudi kwa kuahidi ushirikiano mzuri.
“Waandishi mnafahamu kuwa ninafanya kazi nanyi katika shida na raha, mtukosoe lakini nanyi tukiwakosoa msilalamike,” alisema Mulongo na kuzua minong'ono kutoka kwa wanahabri.
Matukio ya kuuwawa kwa mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, kuteswa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa gazeti hili, Absalom Kibanda ni kati ya mambo yaliyolaaniwa vikali.
Kauli mbiu katika maadhimnisho ya mwaka huu, ni usalama na mazingira bora ya utendaji kazi kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari.
Wakati huo huo, Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi ya Watu wenye Ulemavu (HREDP) inakusudia kuishitaki Serikali kwa kushindwa kuweka mkalimani bungeni.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, hatua hiyo inawanyima watu wenye ulemavu haki yao ya msingi ya kupata habari kutokana na kukosekana mkalimani ndani ya Bunge.
Hayo yalisemwa jana, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Habari Duniani, ambapo Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kilitembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Abubakar Rakesh, alisema kutokana na kutokuwapo kwa mkalimani, kumesababisha watu wenye ulemavu kushindwa kupata habari za Bunge.
“Hata katiba ya nchi inasema kuwa kupata habari ni haki ya msingi ya kila mwananchi, lakini tunashangaa Bunge letu kutotuwekea mkalimani na kusababisha kupitwa na habari nyingi,” alisema.
Habari hii imeandaliwa na Abraham Gwandu, Arusha na Christina Gauluhanga, Dar es Salaam.
KUTOKA GAZETI LA MTANZANIA.
0 comments:
Post a Comment