JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya.
Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.
Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato
cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu
uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira
yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika
mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule
uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.
Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlakaaliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha
20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upyaMatokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.
Aidha,
imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu
uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani
hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya.
Hivyo, Serikali inapenda
kuwahakikishia wananchi kwamba
wa mitihani hiyo.
hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji.
Kutokana
na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya
Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi
karibuni.
Selestine Gesimba
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO
YA UFUNDI
10/05/2013
0 comments:
Post a Comment