Na Hamida Shariff,Morogoro.
WAFANYABIASHARA
wawili wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na kuporwa fedha kiasi cha Sh 2.3
milioni pamoja na simu za mikononi katika tukio la ujambazi lililotokea katika
soko kuu la ndizi la Mwanzomgumu kata ya Bigwa manispaa ya Morog
oro.
Katika tukio
hilo lililotokea Mei 11 majira ya saa 10 jioni pia jambazi mmoja aliuawa na
wananchi baada wenzake kukimbia na bunduki waliyonayo na kumuacha kumuacha nyumba
ambapo alishambuliwa kwa mawe na malungu
mpaka kumuua.
Akizungumzia
tuki hilo Kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa John Laswai aliwataja
wafanyabiashara waliopigwa risasi kuwa ni Hussein Ramadhani (40) mkazi wa
mbarahati kwa jongo jijini Dar es Salaam ambaye alipigwa risasi kwenye goti
mguu wa kulia na Furaha Shomari (30) mkazi wa mwanzo mgumu manispaa ya Morogoro
ambaye alipigwa risasi ya ubavuni na kutokea tumbani.
Kaimu
kamanda huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea mara baada ya mfanyabiashara
Hussein Ramadhani kufika sokoni hapo akiwa na Sh. 2.3 milioni ambazo alitaka
kufanya manunuzi ya ndizi ambapo ghafla walitokea majambazi hao watano wakiwa na
bunduki aina ya SMG na kuwataka wafanyabiashara wote kulala chini huku
wakmlenga mfanyabiashara huyo.
Alisema kuwa
majambazi hayo yalifyatua risasi mbili hewani na baadaye kumlenga
mfanyabiashara huyo na mwenzake kasha kupora fedha hizo pamoja na simu ya mkononi
yenye thamani y ash. 80,000 kisha kikimbia maporini.
Laswai
alisema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mmoja kati ya majambazi hayo
aliwahi kuwa mfanyabiashara wa ndizi sokoni hapo na kwamba polisi wanaendelea
na uchunguzi zaidi ambapo tayari askari wameanza msako wa kuwatafuta majambazi
hayo ambayo yanadaiwa kukimbilia milima ya kinole Mkuyuni.
Aidha kaimu
kamanda huyo alisema kuwa katika eneo la tukio polisi waliokota maganda nane ya
risasi za SMG na hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana na polisi katika
kufanikisha kuwakamata majambazi hayo.
Wakizungumza
kwenye wodi namba moja hospitali ya mkoa wa Morogoro walikolazwa
wafanyabiashara hao walisema kuwa walifika sokoni hapo wakitokea jijini Dar kwa
ajili ya kununua ndizi na muda mfupi kabla hawajafanya manunuzi ndipo
walipovamiwa na majambazi hayo yaliyokuwa na bunduki ambayo ilikatwa kitako.
0 comments:
Post a Comment