BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKENYA WAANDAMANA KUPIGA ONGEZEKO LA MISHARA YA WABUNGE

Wanaharakati wa mashirika ya kiraia wakipinga hatua ya wabunge kujiongezea mishahara Wanaharakati wa mashirika ya kiraia wakipinga hatua ya wabunge kujiongezea mishahara.
 
POLISI wa kupambana na ghasia nchini Kenya walifyatua gesi ya kutoa machozi na mabomba ya maji Jumanne ili kusambaratisha kiasi cha waandamanaji 200 waliokusanyika nje ya bunge wakiandamana dhidi ya madai ya mishahara ya wabunge.
Makundi ya haki za kiraia yaliandaa maandamano yaliopata uungaji mkono kupitia mitandao ya kijamii ili kuelezea hasira za wakenya ambapo wanasiasa wanadai mapema nyongeza ya mishahara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kwa amani hapo Machi 4.

Watayarishaji wa maandamano ya “kulidhibiti bunge” walisema lengo lao ni kusaidia kuwafichua wanasiasa wenye tamaa na walaji rushwa katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa Afrika mashariki.

Waandamanaji waliwanywesha nguruwe damu kwenye milango ya bunge katika mji mkuu Nairobi kama ishara kwa wabunge kuonesha ishara ya “tamaa.”

“Tumesambaza damu ya nguruwe kuonesha kwamba wabunge wana tamaa kama nguruwe” alisema Boniface mwangi kabla ya yeye na waandaaji wengine kukamatwa na polisi.
http://www.voaswahili.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: