Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji
walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar
es Salaam hivi karib
uni.
Na
Mwandishi Wetu.
BAADHI
ya wananchi jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hoja iliyozuka bungeni wiki hii
kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku nchini.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua uamuzi wa
kupiga marufuku kinywaji hicho, watarudia kunywa pombe aina ya gongo ambayo ni
hatari kwa afya zao.
Mkazi
wa Mbagala, Faustine Mwiruka aliyekutwa kwenye baa ya Kisuma, aliiasa Serikali
kutothubutu kukubali kinywaji hicho kupigwa marufuku, kwani ikifanya hivyo
wengi wa wananchi wenye kipato cha chini wataanza tena kunywa gongo na pombe za
kienyeji.
Itabidi
tufanye kama Zambia ambao wamezuia viroba, lakini nchi nzima imejaa
viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose kodi kote
kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na gongo.
Alisema
haingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari, akidai kuwa hata
kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.
"Sisi
tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya gongo
ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa afya
zetu." alisema Mwiruka.
Naye
Ali Hassan mkazi wa Kinondoni kwa Manyanya, alisema, wanaotaka viroba vipigwe
marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana
uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.
Mwandishi
wetu aliyetembelea maeneo ya Ilala Kota Mchikichini alifanikiwakuhojiana na
wakazi wa eneo hilo ambao wengi wao walisema kuwa jambo hilo lililozushwa wiki
iliyopita wanaamini ni njama za wafanya biashara toka nchi jirani ambao
hawaitakii mema Tanzania kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza
pato la Taifa.
Juma
Pingu alisema kuwa haoni sababu ya kupiga marufuku viroba kwakuwa ni pombe ya
wanyonge na kuwataka wabunge kuthamini bidhaa za nyumbani kwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa Konyagi,
David Mgwassa alisema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na mchezo mchafu wa
kuharibiana jina sokoni kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari vya hapa
nchini, kampeni inayoendeshwa na makampuni yenye uhusiano na makampuni makubwa
ya pombe duniani yasiyo penda, nchi za afrika zizalishe pombe zake, bali
ziendeleee kununua kutoka Ireland, wales. Kenya and uingereza.
Wadau
hao wa Pombe nchini walifikia uamuzi wa kutoa maoni hayo baada ya kuona kuwa
kinywaji chao Kiroba kinapigwa vita lukuki kwenye magazeti.
Huwezi ukahusisha
viroba na piki piki, kwani nchi hii ina piki piki laki tatu, na wananchi
million 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi ?.
0 comments:
Post a Comment