BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI MEMBE ATUHUMIWA VURUGU ZA MTWARA.

HIKI NDIVHO ALICHOANDIKA ZITTO KUHUSU WAZIRI MEMBE KATIKA UKURASA WAKE WA TWEETTER.Membe: Malawi isiguse mpaka wa Tanzania
WAZIRI MEMBE.
 
Jackson Odoyo, Dar es Salaam
WAKATI vurugu za Wananchi wa Mtwara zikiendelea na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo Mama mjamzito, huku Askari wanne wakifariki Dunia  katika ajali ya gari walipokuwa wakitokea Nachingwea kuelekea Mtwara kutuliza vurugu hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Bernard Membe anatuhumiwa kuhusika katika vurugu hizo.

Waziri Membe anakuwa mtu watatu kuhusishwa na vurugu hizo ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutup
iwa lawama kedekede kwamba ndiye mfadhili mkuu wa vurugu za Mtwara.

Hata hivyo tuhuma hizo za Zitto ziliyeyuka baada ya watu mbalimbali waliotoa tuhuma hizo kukosa ushahidi, huku serikali pia ikikosa ushahidi wa kumtia Mbunge huyo wa Chadema hatiani kutokana na vurugu hizo.

Wakati watu wakiendelea kutafakari juu ya tuhuma hizo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Haruna Ibrahim Lipumba naye akarushiwa lawama kama hizo kwamba ndiye mchochezi mkubwa wa ruvugu za Mtwara.

Leo hii Waziri Membe ametupiwa lawama hizo kutoka kwa wabunge wa CCM ambao walisema kwamba Waziri Membe ndiye chanzo cha vurugu hizo na kufanya idadi ya wanasiasa waliotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo kufika watatu.

Tuhuma za kwamba Membe anakabwa koo na wabunge wa CCM kwamba anahusika katika vurugu za Mtwara zilinaswa na Habarimpya.com kutoka vyanzo vya habari ndani ya CCM.

Mbali na Habarimpya.com kudokezwa juu ya tuhuma hizo za Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini pia alianika tuhuma hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Tweeter.  

Akichati na watu mbalimbali akiwemo @Carol Ndosi, aliyemwambia Zitto kwamba, "Kwa maoni yangu, bomba sio tatizo la msingi. Bomba Ni alama ya kuwaunganisha tu wananchi"alisema Carol Ndosi alipokuwa akichati na Zitto.

"Badala ya kutafuta suluhisho la kudumu, Mtwara tunatafutana. Rais analaumu wanasiasa. Waziri Nchimbi analaumu wanasiasa. Kweli? Ndio chanzo? Hatuishi vituko sisi, sasa wabunge wa CCM wanasema Waziri wa Mambo ya Nje ndio anachochea vurugu Mtwara. Ilikuwa Zitto, kisha Lipumba...."alisema Zitto Katika Ukurasa wake wa Tweeter.  
Chanzo http://www.habarimpya.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: