BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFISA HABARI AVAMIWA NA MAJAMBAZI DAR ES SALAAM

 Operl 2Edward na Mkewe Mtarajiwa Elizabeth, siku ya send Mjini Same, wikiendi iliyopita. Operl 3Edward akiwa wodini Moi.
Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola  amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.

Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.

Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja  mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.
 
 Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa  Elizabeth.

Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: