MATUMIZI
ya Shirika la Umeme (Tanesco) kwa mwaka ujao wa fedha yameiweka
Serikali njia panda hasa baada ya kutakiwa kutafuta fedha hizo nje ya
bajeti.
Kamati ya Bunge ya Bajeti imeweka wazi kuwa fedha zilizotengwa na
Serikali kwa ajili ya matumizi ya shirika hilo linalotegemea zaidi
ruzuku ya Serikali, ni ndogo kuliko mahit
aji halisi ya Shirika hilo kwa
mwaka.
Kutokana na hali hiyo, Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi
Magharibi, Andrew Chenge na wabunge wameungana kuitaka Serikali
kutobadilisha matumizi ya fedha zilizopangwa na Bunge katika bajeti
yake, huku wakiitaja Wizara ya Nishati na Madini kuwa moja ya wizara
zilizotumia fedha zaidi ya bajeti waliyopangiwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Chenge, Wizara ya Nishati na Madini katika mwaka wa
fedha unaoisha, ilipangiwa kutumia Sh bilioni 76.99 lakini ikatumia Sh
bilioni 148.42, sawa na ongezeko la Sh bilioni 71.43.
Wizara nyingine
zilizotumia fedha zaidi ya bajeti ilizopangiwa ni Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, ambayo ilipangiwa kutumia Sh bilioni 80.6
lakini ilitumia Sh bilioni 112.08 sawa na ongezeko la Sh bilioni 31.47.
Pia Wizara ya Afya, lipangiwa kutumia Sh bilioni 219.36 lakini ilitumia
Sh bilioni 246.71, sawa na ongezeko la Sh bilioni 27.35.
Deni la Taifa
nalo, lilipangiwa kutumia Sh trilioni 1.9, lakini lilitumia Sh trilioni
2.5 sawa na ongezeko la Sh bilioni 624. Akizungumzia hali hiyo juzi
bungeni, Chenge alisema katika hali ya kushangaza wizara hizo zimetumia
fedha zaidi ya zilizoidhinishwa na Bunge.
Ili kukabili hali hiyo, Chenge
akaitaka Serikali, itakapotaka kuongeza fedha zaidi ya zilizoidhinishwa
na Bajeti, kwa maana ya kuhamisha mafungu, iwasiliane kwanza na Kamati
yake.
Matumizi ya Tanesco nje ya bajeti Kuhusu Tanesco, Chenge alisema;
“Ni muda mrefu sasa Shirika hili limekuwa likitumia fedha nyingi kwenye
ununuzi wa mafuta kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.
“Kamati imebaini kuwa Serikali imekuwa ikitenga fedha kidogo kwa ajili
ya kuendesha Shirika hili, hali inayosababisha kufanyika kwa uhamisho wa
fedha kutoka katika maeneo mengine kwa ajili ya kupeleka Tanesco,”
alisema.
Ili kuzuia hali hiyo, Chenge alisema Kamati yake ilikutana na
Tanesco pamoja na Wizara ili kupata taarifa za gharama halisi ya Tanesco
kwa mwaka ujao wa fedha, ambao shirika hilo limetengewa Sh bilioni 273.
“Katika kikao hicho, ilibainishwa kwamba kwa mwaka 2013/14, Tanesco
itaendesha mitambo kwa asilimia 78, na kwa mpango huo, Tanesco itatumia
Sh trilioni 1.2,” alisema Chenge na kuongeza kuwa mitambo hiyo ikiwashwa
kwa asilimia 100, shirika hilo litatumia Sh trilioni 2.2.
Zigo la
Serikali Badala ya kujadili wapi fedha hizo zitapatikana, au kutoa
nafasi ya Wizara kukutana na Kamati kutafuta fedha hizo, Chenge alitaka
Serikali itafute fedha hizo sehemu nyingine bila kugusa bajeti.
“Kamati
inashauri kuwa fedha hiyo ipatikane bila kuathiri Bajeti ya Serikali,”
alisema.
Wakati wa kuchangia bajeti hiyo, wabunge wengi pia walisimamia
msimamo huo, bila kuitaja Tanesco, wakataka Serikali isibadilishe
matumizi ya fedha zilizopangwa katika bajeti, na wengine kufikia hatua
ya kutaka Sheria ya Bajeti, ili kuidhibiti Serikali isihamishe vifungu. CHANZO HABARILEO

0 comments:
Post a Comment