BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BREAKING NEWS: M 2THE P AWASILI TANZANIA KWA AJILI YA KUMZIKA NGWAIR, SIKILIZA HAPA ALICHOKISEMA AKIWA BONGO

m 2 the p
Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo (June 6).Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea.

“Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,” alisema.
Share on Google Plus

About Anonymous

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: