BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DIAMOND ATOA SIRI YAKE NAA MANGWEA.

DIAMOND.
 https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcTcbPsmB8oL0NdNY9ZTMuOtFcF-881836OfLxvYzL9xEVxaoG1Z5Q
WAKATI watu mbalimbali maarufu nchini, hususan wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), wakiendelea kutoa historia ya mahusiano yao na aliyekuwa msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Albert Mang
wea, msanii maarufu wa muziki nchini Nassib Abdul (Diamond Platnumz) amevunja ukimya na kutoa siri yake na marehemu Mangwea.

Akielezea hisia zake pamoja na mipango mingi aliyokuwa nayo kuhusu kufanya kazi ya muziki na marehemu katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond alisema kwamba alijaribu kufanya kazi ya pamoja na msanii huyo lakini kwa bahati mbaya kazi zote zikaharibika.

"Kinacho niumiza ni jinsi tulivyo jaribu kutengeneza HIT bila mafanikio yaani siyo nilizo mshirikisha hata zile alizo nishirikisha na tuka amua kuplan kutengeneza nyingine akirudi kutoka Afrika Kusini, lakini haikuwezekana yani mungu alimpenda zaidi":alisema Platnumz.

Kila binadamu huwa na jambo lake muhimu ama siri ya mafanikio baina yake na mtu mwingine ambayo pengine si rahisi kuizungumzia hadharani ama wakati wowote, lakini inapotokea mmoja kati yao akifariki dunia anayebaki duniani hujikuta akitoa siri hiyo.

Hatua ya Binadamu kuamua kutoa siri yake na mwenzake wakati wa msiba wa mmoja wao inaweza ikawa na tafsiri nyingi lakini ukweli nikwamba huzuni na machungu ya kuondokewa na mtu muhimu kwake aliyekuwa akitarajia kufanya naye jambo flani muhimu ndiyo husababisha mtu huyo kutoa siri.R.I.P Mgwea.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: