BAADA
ya kutoka kwenye Mochwari ya serikali ya Hillbrow Johannesburg, mwili
wa Ngwea ulihifadhiwa hapa ambako pia msafara wa kwenda kumuaga ndio
ulianzia hapa.
Ni zaidi ya Watanzania 50 waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu
Ngwea akiwemo Msanii Bushoke, Mwamvita Makamba, Kinje Ngombale Mwiru
pamoja na Watanzania wengine waliokuja kutembea na wanaoishi na kufanya
kazi Afrika Kusini.
Marehemu Ngwea alifariki dunia may 28 2013 Johannesburg South Afrika
alikokuja kufanya show, ambapo kilikua ni kifo cha ghafla kwa sababu
usiku kabla ya kulala aliagana vizuri na Watanzania wenzake kijiweni
tena akaahidi kurudi Afrika Kusini baada ya kipindi cha Ramadhani.
Kabla ya kifo chake tayari Ngwea alitakiwa kurudi Tanzania lakini
akaahirisha safari yake mara tatu mfululizo ili aendelee kuwepo Afrika
Kusini ambako alimwambia Bushoke kwamba amepata mtu wa kumlipia ada
hivyo angerudi Afrika Kusini hivi karibuni ili aanze masomo ya muziki.
.
Gari
la Ubalozi wa Tanzania lililotoka Pretoria likiwa na Mwakilishi wa
Ubalozi huo, hapa lipo kwenye msafara kuelekea kanisani kuuaga mwili wa
Marehemu.
.
Msafara wa magari ya Watanzania mbalimbali.
Baadhi ya Watanzania wakiubeba mwili wa Marehemu kuuingiza ili kwenda kuagwa.
.
Josh
Kalisa, Habibu Awesi ambae ni mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania Afrika
Kusini, Kinje Ngombale Mwiru na Mwamvita Makamba wakiwa nje ya kanisa
alikoagwa Marehemu Ngwea Johannesburg June 3 2013.
.
.
Watanzania wakiingia Kanisani kuaga.
.
.
.
Magari waliyokuja nayo Watanzania mbalimbali.
Baada ya kuaga, mwili ulipakizwa kwenye gari ili kupelekwa Airport.
Ndani kanisani.
Huyu
ni Ramadhani, ndio Mtanzania ambae alikua anamuendesha Ngwea mara
nyingi sana kipindi hiki alipokuepo Johannesburg ambapo usiku kifo
kilipotokea, walikoswakoswa kwenye ajali kadhaa barabarani…. hapa alikua
anasali kwa ajili ya Marehemu.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania akiongea baada ya sala ya kumuombea Marehemu Kanisani.
.
.
.
.
.
.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment