Wasanii wanaaga sasa.
Sehemu ya waombolezaji waliokwenda wakimuaga marehemu Ngwea katika viwanja vya Leaders Club leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema (BAVICHA), John Heche wa tatu kutoka kushoto akijadiliana na viongozi wenzake waliokwenda kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea leo viwanja vya Leaders Club leo.
Fid Q na Feroos wakibadilishana mawazo katika viwanja vya Leaders Club leo.
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan kulia, akijadiliana jambo na mjukuu wa Julius Kambarage Nyerere, Sofia Nyerere na ndugu yake kushoto kwake katika viwanja vya Leaders Club leo.
Waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakijadiliana jambo katika viwanja vya Leaders Club leo.
Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakionekana katika viwanja vya Leaders Club leo.
Sehemu ya
waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea ikiwa kwenye
pilikapilika za kutaka kumuona kwa karibu msanii Diamond, hivyo kuvunja
utaratibu mzima, wakati shughuli hiyo inaelekea mwishoni katika viwanja
vya Leaders Club leo.
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
Marehemu
Albert Mangwea ameagwa leo katika Viwanja vya Leaders Club na kuelekea mkoani
Morogoro kwa ajili ya mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho katika Makaburi
ya Kihonda.
Aidha
viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa walihudhuria katika viwanja
vya Leaders Club, wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzam.
Msanii
Nassib Abdulmalick ‘Diamond’ alimuelezea marehemu Ngwea kama moja ya wasanii
wenye uwezo mkubwa wa kuimba, huku akiweza kuishi kwa upendo na wasanii wote,
tangu alipojiingiza kwenye muziki.
“Nimeguswa
sana na msiba wa Ngwea, naamini pengo lake haliwezi kuzibika, maana jamaa
alikuwa na uwezo mkubwa mno katika tasnia hii, akitamba na nyimbo nyingi
zilizowafurahisha watu wote,” alisema Diamond.
0 comments:
Post a Comment