BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JE WAJUA KILICHOJILI KATIKA MAZISHI YA MWANAMUZI, ALBERT KENETH MANGWEA MOROGORO ?.

Mama mzazi wa marehemu Albet Mangwea Bi. Denisia Mangwea akisali mbele ya mwili wa mwanae muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuaga kabla ya kuanza msa
fara kuelekea makaburi ya Mtakatifu Monica Kihonda ambapo mazishi yalifanyika mkoani Morogoro jana.
Umati wa watu katika Manispaa ya Morogoro wakiwa wametanda barabara kuu ya Old Dar es Salaam kwa lengo la kushuhudia gari lililobeba mwili wa msanii Albert Keneth (28) eneo la stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro wakati wa msafara wa kuelekea katika makaburi ya Mtakatifu Monica Kihonda kwa ajili ya mazishi yalifanyika mkoani Morogoro jana.



Na Lilian Lucas,Morogoro.
HATIMAYE  safari ya mwisho ya aliyekuwa masanii wa kizazi kipya Albert Magwea maarufu kama Ngwea imehitimishwa kwa maelfu ya wananchi wa mkoa wa Morogoro, jiji la Dar es salaam na maeneo mengine ya jirani wamejitokeza kuaga mwili wa msanii huyo baadaye kushiriki maziko katika makaburi ya kanisa katoliki la mtakatifu Monica yaliyopo Kihonda mjini Morogoro.

Wananchi hao waliojitokeza kwa wingi tangu kupokelewa kwa mwili wa msanii huyo siku ya jumatano majira ya saa 11.30 ukianzia maeneo ya Mikese kupitia Msaavu ukitokea Jijini Dar es salaam, walijitokeza pia katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo ibada ya mazishi ilifanyika na baadae watu kuanza kuaga mwili huo.

Hata hivyo mazishi hayo yaliingiliwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii a maigizo ambao walitia dosari, baada ya baadhi yao kuchelewa kuingia katika uwanja wa Jamhuri, akiwemo TID, Jini Kabula, Dokii, Juma Nature, na kundi lake  na wasanii wengine, kwa kusababisha kushangiliwa na wananchi waliofika uwanjani hapo.

Aidha magari ya chama chama cha Mapinduzi nayo yaliingia uwanjani hapo, ingawa hakukuwa na msisimko wa kushangiliwa kama ilivyojitokeza awali kwa gari lililokuwa na bendera ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, hali iliyoonesha wengi waliofka kuhudhuria msiba huo walikuja kwa nia ya kuwaona wasanii na viongozi wa vyama vya kisiasa na sio kuomboleza huku na baadhi ya wasaii na vongozi wa kisiasa wakiingia kwa nia ya kujionesha kwa wananchi.

Hali hiyo ilifanya ibada iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo ikiendeshwa na Paroko wa kanisa katoliki, Parokia ya Mt Monica, Octavian Msimbe, kuingiliwa kwa kelele hizo za wananchi mara kwa mara, ingawa haikusababisha ibada kusimama.

Aidha siku ya kuwasili kwa mwili huo wa msanii Ngwear kutoka Dar es salam,wananchi pia walisimamisha baadhi ya magari ya wasanii akiwemo msanii, Dully Sykes, ambaye baada ya kufika eneo la Msamvu kulikokuwa na mkusanyiko mkubwa wa waananchi, baadhi yao walisimamisha gari yake na kuzuia isiendelee na safari, huku wakipiga kelele za kuita jina la Dully na kusukuma gari hiyo kwa mikono.

Akiongea wakati waibada hiyo, Paroko msaidizi wa Kanisa la St Monica Padre Petter Luanda,aliwataka wananchi kutohuzunika kwa kupitiliza kuhusiana na kifo cha msanii huyo, kwani wana nafasi ya kufurahi tena pamoja naye mbinguni, na kwamba kifo hicho ni kumbukumbu ya kifo cha kila mwanadamu kwa kujiweka tayari kwa vle hawaijui siku wala saa.

“Hakiwezi kutusubiri  tuwe wazee wa miaka themanini,tunapomsinikiza mwenzetu tujue siku yingine itakuwazamu yetu, na tujiandae kwa siku hiyo, jiulize kama mimmi ninekufa leo, ningekuaje, ninngekuwa katika hali ya kukubalika mbinguni au kwenda kwenye adhabu?.

leo ndio siku ya kufanya uamuzi wa kukiondoa kinachokufanya uende kenye adhabu na kukufanya kukubalika kwenda mbinguni, tujichunguze sasa uhusiano wetu na Mungu na kujirekebisha,”Alisema Paroko huyo msaidizi.

Maishi hayo mkoani Morogoro yaliongozwa na MKuu wa Mkoa Joel Bendera, na waziri Kivuli wa Habari Utaduni na Michezo kutoka Kambi  ya Upinzani Bungeni, Joseph Mbilinyi, Sugu,wawakilishi wa wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya Habari,Utamaduni na michezo, Sugu  alisema ifike wakati Serikali na wadau wegine waangalie maisha ya wasani wakati  wa maziko, yaendane na maisha halisi ya wasanii wakiwa hai.

Mwakilisi wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mourice Masalla aliwaasa wasanii kutumia msiba huo kuwa na hofu ya Mungu, huku  Msanii Masanja Mkandamizaji alipohojiwa akiwanyumbani kwa marehemu eneo la Kihonda, akieleza kushangazwa na umati mkubwa ukiojitokeza kumsindikiza Ngwear na kwamba kama wangekuwa wanajitokeza hivyo wakati wa matamasha na kazi zao, na kuwaunga mkono, basi huenda umaskini kwa wasanii usingekuwepo. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera, alieleza Mkoa ulivyopokea kwa msikitiko msiba wa Ngwear akiwa ni kijana mahiri anayeweza kuigwa na wenzake, na kwamba umati uliojitokeza umeonesha namna marehemu alivyokuwa karibu na watu, na alivyokuwa karibu na wasanii wenzake na kuahidi Serikali kuendelea kulinda kazi za wasanii ili waweze kufaidika.

Kwa upande wake katibu mtendaji wa bodi ya Filamu na mwakilishi wa wizara ya habari,vjana ,utamaduni na michezo Joyce isso na Kaimu katibu mtendaji wa baraza la sanaa la  Taifa  BASATA Godfrey Mngereza walisema serikali inatambua mchango wa Ngwea na kuwaasa wasanii wanaonuia kuiga mazuri aliyoacha marehemu ikiwa ni pamoja na kuyaendeleza ili kumuenzi.

Waliwaasa wasanii kuendelea kushirikiana na serikal katika kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji kama cha marehemu angwea ili muziki na sanaa viendelee mbele,na kuwa njia ya kuwaenzi waasisi wa muziki na fani nyingine za utamaduni.

Marehemu Albert Keneth Mangwea alizaliwa mwaka 1982 katika hospitali y Mkoa wa Mbeya, akiwani mtoto wa 10 wa mzee Keneth Mangwea na mama Denisia mangwea na alipta elimu ya msingi shule ya msingi Bungo kuazia mwaka 1990, na mwaka 1994 alihamia mkooani Dodoma ambapo alihitimu mwaka 1997 na baadaye alijiunga sekondari ya Mazengo ambapo alihitimu mwaka 2000.

Mwaka 2002 alijiunga na chuo cha sana Bagamoyo na alikuwa mhamasishaji wa vikundi mbalimbali vya wasanii ikiwemo kundi la ChembaSquard akiwa kama muasisi wa kundi hilo, na aliasarifi kwenda nchini Afrika ksini mnamo Machi 26 kwaajili ya shughuli za kimuziki kabla ya mei 25 alipo0fariki dunia, na kwa mjujibu wa familia ya marehemu, hakuacha mke wala mtoto.

Mwili wa marehemu Albert Magwear umezikwa katika makaburi ya kanisa la ST Monica yaliyopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.

Hata hivyo taarifa zaidi zilibinisha Msanii huyo kuwa na mchumba raia wa Canada, ambahye pia alikuwepo katika mazishi hayo.Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Mungu akiweke roho ya Marehemu Albert mahali pema peponi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: