Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe Dar es Salaam.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chakawe amesema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Chikawe alizungumza Dar es Salaam jana kuwa, ikiwa
mchakato wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama
inavyokusudiwa na rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote
bila mabad
iliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.
iliko, muda utakaobaki utatosha kuandaa Katiba ya Tanzania Bara.
“Watu wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu
itapita bila mabadiliko na kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka
Desemba inatosha kabisa kuandaa Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda
katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na Katiba Mpya,” alisema na kuongeza:
“Tunaweza kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya
Katiba, lakini safari hii tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee
wakashiriki katika kuandaa Katiba hiyo.”
Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema kutokana na
muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya kukusanya maoni
kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake ikaandaa rasimu
na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza ya Katiba kabla
ya kupata Katiba Mpya.
Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa
kukamilika Aprili mwakani.
Chikawe anasema kuanzia hapo Serikali inaweza
kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Tanzania
Bara kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo hatua ya kwanza ikawa ni
kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya Katiba kwa miezi miwili na
baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba jambo litakaloifanya ipatikane
mapema.
Waziri Chikawe alisema kinachotakiwa sasa ni
kujiandaa kwa Tanzania Bara kuwa na Katiba yake ambayo itatumika kwa
ajili ya mambo mbalimbali, ukiwamo Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Waziri huyo aliwatoa hofu Watanzania kwamba hakuna
mpango wa kumwongezea muda wa uongozi, Rais Jakaya Kikwete kama ambavyo
imekuwa ikielezwa kwani Serikali ina uhakika kwamba kila kitu
kitafanyika katika muda uliopangwa.
Siku chache zilizopita Mwenyekiti wa CUF, Profesa
Ibrahimu Lipumba alikaririwa akisema kuwa Serikali ina mpango wa
kumwongezea Rais Kikwete muda wa kuongoza.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Wakati Chikawe akitoa kauli hiyo, habari kutoka
ndani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), zinasema kutokana
na mapendekezo ya kuwapo kwa Serikali tatu, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema anaandaa “kitu muhimu” ambacho
atakiwasilisha bungeni siku chache zijazo.
Chanzo MWANANCHI
Chanzo MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment