ZOEZI la kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya
marehemu Albert Mangwea aliyefariki Dunia nchini Afrika Kusini Mei 28
umesitishwa huku umati mkubwa ukiwa haujamaliza kuuaga.
Kitendo cha Kamati ya maandalizi kukatisha zoezi la kuuaga mwili wa
marehemu kwa sababu ya muda uliopangwa kukamilika iliwashangaza mamia ya
watu waliokuwa kwenye foleni ya kusubiri kupata nafasi ya kutoa hesh
ma
zao za mwisho mbele ya Jeneza la Mangwea.
Zoezi hilo liloanza saa 2:30 asubuhi imesitishwa saa 6:30 mchana kwa
saa za Afrika Mashariki na Kati, na msafara ukiongozwa na Askari wa
Jeshi la Polisi pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama waliokuwa katika
Viwanja vya Leaders Club.
Barabarani Asakari wa Kikoso Cha Usalama Barabarani pia walijiapanga
vizuri kuhakikisha kwamba msafara wa mwili wa marehemu unapita vizuri
katika maeneo yaliokuwa yamepangwa kuelekea mjini Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr Blue alifika katika viwanja hivyo
akiwa amechelewa na kukosa muda wa kuuaga mwili wa Mangwea lakini
alipokutana na mashabiki wa muziki wake aliweza kusimama na kuwapa pole.
Mwili wa Mangwea hivi sasa uko safarini kuelekea Mjini Morogoro
ambapo utalala nyumbani kwa mama yake na kesho uwakazi wa Mji huo pia
watapata nafasi ya kutoa heshma zao za mwisho.
Endeleeni
kufurahia na kufuatilia taariza za mazishi ya Mangwea hapa hapa
Habarimpya.com pia tunaomba maoni yetu kuhusu taarifa mbailmbali za
Habarimpya.com
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment