BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

PROFESA HARUNA LIPUMBA:ATOBOA SIRI YA URAIS WA JAKAYA KIKWETE..

 
NILIKUWA MSHINDI WA TATU 2010 NA RAIS KIKWETE ALISHIKA NAFASI PILI. PROFESA LIPUMBA.

Dar es Salaam,Tanzania
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na “kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita. Profesa Lipumba alitob
oa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa, miezi kadhaa iliyopita.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema “wenzetu wameanza kujipanga” kuelekea 2015.  

Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong’ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete. Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini. 

Hata hivyo alisema inawezekana video hiyo imechakachuliwa kwa kuungaunga vipande vya matamshi wanavyovitaka badala ya hotuba nzima.  

Hata hivyo, video iliyotazamwa na waandishi wa habari hii, katika video hiyo Profesa Lipumba anaeleza alivyoshika nafasi ya tatu nyuma ya Rais Kikwete huku matokeo yakionyesha Dk Slaa kuongoza.

Katika tukio hilo, Sheikh Baseleh ndiye anayeanza kuzungumza huku akisoma kipande cha gazeti lililomnukuu Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, Dk. Mary Nagu, akizungumzia mchakato wa katiba, kwamba Tume ya Katiba “haitazingatia maoni ya wachache”, na kwamba mambo ya dini yasiingizwe kwenye katiba.  

Katika ufafanuzi wake, Sheikh Basaleh anasema Dk. Nagu alizungumza mambo haya mbele ya waumini wa Kanisa la Chang’ombe kwenye uzinduzi wa kwaya na kwamba miongoni mwa mambo ambayo yanaitwa ya kidini yasiyotakiwa kuingizwa kwenye katiba ni Mahakama ya Kadhi Mkuu.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments:

Anonymous said...

Ni kweli Lipumba alishika nafasi ya tatu. Ila nafasi ya kwnza mshindi hakuwa JK.