ENZI za utawala wa Rais Mwalimu Julius Nyerere kulikuwa na uvumi kuwa Tanzania ilikuwa na idara nzuri sana ya TISS hata na kudaiwa kuwa iliwahi kushika nafasi ya tatu kwa upelelezi duniani.
Kwa upande mmoja naweza kuona ukweli wa hili nikijaribu kulinganisha TISS ya enzi za Nyerere na TISS ya enzi hizi, nakumbuka wapelelezi wa enzi hizo wengine waliweza hata kuwa kama vichaa kwa kuvaa nguo chaf
u ili waweze kukamilisha upelelezi na wakafanikiwa hata kuwakamata makaburu waliokuwa wanakuja nchini kutoka Afrika kusini kwa njia za pori.
Lakini siku hizi wasomali wanaingia nchini na kutoka wachache ndo kuwa wanakamatwa tena na polisi kwa kupewa taarifa na raia wema na sio TISS.
Naomba michango yenu wana bodi kuhusu jambo hili ukilinganisha na haya matukio yanayotokea kwa sasa.
CHANZO http://www.udakuspecially.com
0 comments:
Post a Comment