POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanik
iwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...
Kamatakamata hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa
Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo
Kariakoo, jijini Dar ambalo machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa
wateja.
Katika hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa
na makahaba hao ilitimua mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria
kusafisha eneo la Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.
Baadhi ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika
wakisema kuwa wakukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao
kwa vile wanavaa kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati
wowote.
“Sisi kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa,
watavaaje kimitego mbele yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati
huo?” alisikika akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita
kawaida.
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa makahaba hao
halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo, kahaba mmoja aliuliza:
Una maswali mengi kwani we ni polisi?
Mei 24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye
Mahakama ya Jiji na kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe
mbele ya Hakimu Timoth Lyoni.
Waliosomewa
mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi), Niyonkuru
Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na Wabongo
35.
Wote
walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya
kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
0 comments:
Post a Comment