Richard Bukos na Issa Mnally
Tukio hilo lililoshuhudiwa na
wanahabari wetu majira ya usiku jirani na msikiti huo uliopo nyuma ya
Corner Bar, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke huyo na wenzake
walikamatwa na baadhi ya vijana waumini wa Kiislamu waliokerwa na
kitendo cha wao kutoa huduma haramu ya ngono maeneo hayo.
WENZAKE WATOKA NDUKI
Baada ya
wenzake kufanikiwa kutoka nduki mithili ya mwanariadha Usai Bolt wa
Jamaika, mwanamke huyo alishuhudiwa akila bakora kisha akapelekwa katika
Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar akaunganishwa na wengine waliokamatwa
usiku huo.
Ilielezwa kuwa wanawake hao wamekuwa wakiuza miili kwa wanaume karibu na msikiti huo na pembezoni mwa baa hiyo.
Ilisemekana
kuwa kumekuwa na kawaida ya wanawake hao kusimama maeneo ya nyumba hiyo
ya ibada na kufanya biashara hiyo huku wakichafua mazingira kwa kutupa
ovyo kondomu na kujisaidia maeneo hayo.
NGUO YA NDANI YAMVUKA
Wakati
mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga
kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.
NI KERO
Kutokana
na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti
huo, waliamua kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi
hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo
hicho cha polisi.
“Tumeamua
kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa,
wanakojoa na kutupa kondomu hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja wa
vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia
mapaparazi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu
kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu
ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.
KUNA KISA NA MKASA
Alisema
kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa
akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose
kuhudhuria swala siku hiyo.
BOFYA HAPA KUSIKIA MAHOJIANO
Gazeti hili liliambatana na vijana hao hadi polisi ambapo lilipata nafasi ya kuzungumza na mwanamke huyo.
Risasi Mchanganyiko: Mama kwani wewe unaitwa nani na kwa nini unajiuza eneo lile ?.
Mwanamke:
Naitwa Zulfa, unajua maisha ni magumu hata ninyi mnajua. Ni kweli mimi
ni mke wa mtu lakini mume wangu hana kazi hivyo kuliko kulaza watoto
njaa naogopa watakufa.
Risasi Mchanganyiko: Mume na watoto umewaacha wapi?
Zulfa: Mume naye anabangaiza mtaani, watoto wangu wawili nimewaacha nyumbani Manzese wamelala.
Risasi
Mchanganyiko: Kwa nini usitafute njia nyingine ya kutafuta kipato kuliko
kujiuza kwa sababu unahatarisha maisha na haya magonjwa ya siku hizi ?.
Zulfa: (kwa ukali), acheni maswali yenu kama mna hela nipeni nitaacha.
AINGIZWA LOKAPU
Hata
hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu
aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe
na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.
NI SIKIO LA KUFA
Habari
zilizolifikia gazeti ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa
na kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini
ya shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado
wanaendelea na biashara hiyo maeneo hayo.
DAR INATISHA
Biashara
haramu ya ngono imekuwa kwa kasi ya ajabu jijini Dar na utafiti wa mwaka
juzi ulionesha kuwa kulikuwa na wanawake wanaojiuza zaidi 7,500 lakini
kwa sasa ni maradufu, chanzo kikielezwa ni ukosefu wa ajira.
NA GLOBAL PUBLISHER
About mtanda blog
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment