Amina Juma.
MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ.
MCHUMBA wa marehemu, Fortunatus Msofe, ambaye ni mmoja wa wapiganaji wa JWTZ, waliofia Darfur, ameondoka kwenda Tanga kumzika mwenza wake huyo.
Mwanamke huyo Amina Juma, amekataliwa na ndugu wa
marehemu ambao wameifunga kwa kufuli nyumba inayodaiwa kuwa amejenga
marehemu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Amina alisema
ingawa awali alikata tamaa ya kumzika mwenzake, lakini jana aliamua
kwenda Tanga kuhudhuria mazishi na kwamba hatua hiyo ilik
uja baada ya kujishauri sana.
uja baada ya kujishauri sana.
Baba wa marehemu, Wilbad Msofe aliiambia gazeti
hili kutoka Kange, Tanga kuwa alishangazwa na hatua ya Amina
kutowafahamisha kuhusu msiba huo.
Alisema hiyo ndiyo sababu za yeye kuamua kutaka mwanawe apelekwe Kange kwa mazishi.
Akizungumza na Mwananchi akiwa njiani kwenda
Kange, Amina alisema: “Nilikuwa ninataka sana kumzika mwenzangu lakini
ile hali ilikuwa imenichanganya pamoja na kwamba nilishauriwa, sasa
nimekata shauri nakwenda Tanga.
“Najua kuna kitu hapa, lakini ‘Fortu’ kwa kuwa
nilikuwa naye, na wana ndugu wa upande wa wake wameshanikana, mimi
nitamzika tu mwenzangu na kurudi,” alisisitiza.
Miili ya wapiganaji hao iliagwa jana katika Makao
Makuu ya Jeshi, yaliyoko Upanga na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni
Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, makamanda na
wanajeshi walishiriki kuwaaga wanajeshi hao.
Akizungumza kwa masikitiko na huku sauti ikiwa
imemkauka kutokana na kulia muda mrefu, Amina alisema: “Siwazii
mtafaruku uliopo, moyo umenituma kwenda kumzika mume wangu, niliwaza
usiku kucha na leo (jana) Jumatatu asubuhi nikaamua kwenda Tanga.”
“Msofe amekufa tulikuwa tuna mipango mingi,
tulipanga harusi kubwa lakini haikuwahi kufanyika, niliongea naye
alfajiri ya Jumamosi ya Julai 13, akaniambia tutaongea baadaye maana
wanakwenda kwenye operesheni...
“Unajua tuliishi maisha ya kipekee sana
tulipendana kiukweli hata majirani tuliokuwa tukiishi nao Mbezi na
Visiga wanajua hilo na wengi walikuwa wakinisihi sana nisije kumuudhi
huyu kijana.
Baadaye akiwa Tanga alisema: “Nafsi yangu inaniuma
sana, yaani kila muda na saa zinavyozidi kwenda.
Alisema hatua ya wakwe zangu kudai kutonitambua si ya kiungwana. MWANANCHI.
Alisema hatua ya wakwe zangu kudai kutonitambua si ya kiungwana. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment