CHEZEA WANAWAKE WEWE !!!!, HIKI NDICHO KILICHOMKUMBA MSANII MASAI NYOTAMBOFU KUACHWA KAMA MTOTO WA KOBE NA MAPENZI WAKE NI HIKI HAPA.
MWIGIZAJI wa Bongo Movies kwa upande wa vichekesho hapa nchini, Gilliady Severine maarufu kama Masai Nyota Mbofu ameueleza mkasa uliowahi kumkumba baada ya tukio la kuachwa kwa kejeli na dharau na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja katika kipindi kingumu chaa kimaisha.
Akizungumza na blog ya www.jumamtanda.blogspot.com kwa njia ya simu kutoka Tanga, Nyotambofu alisema kuwa tukio hilo haliwezi kulisahau katika maisha yake kutokana na kitendo hicho alichokiita sio cha kibinadamu hasa kwa watu waliowahi kuonyeshana upendo wa hali ya juu.
Nyotambofu ambaye kwa sasa anatengeneza video ya wimbo wake mpya na msanii mkali wa bongo flova, Richie Mavoko alibain
ishaa tukio hilo kuwa hawezi kulisahau tangu alipoingia tasnia ya sanaa ya uigizaji na muziki.
“Katika maisha yangu nakumbuka sana tukio la kuachwa kwa kejeli na dharau na mpenzi wake niliyezaa naye mtoto mmoja hasa kipindi ambacho sikuwa na pesa na kuishi maisha ambayo sikufikii siku moja naweza kupata adha ya kulea motto mdogo”. Alisema Masai Nyota Mbofu
Hilo tukio bado linaniumiza moyo wangu mpaka sasa kwa sababu alinidanganya kuwa mtoto wangu niliyezaa naye amefariki dunia !, eti mimi nisiendelee kumsumbua ili yeye apate muda wa kustarehe na mpenzi wake mpya baada ya kunitosa. Alieleza Masai Nyotambufu.
Mama wa mtoto huyu aliyemtaja kwa jina moja la Happy,
anasema kuwa akikumbuka tukio hilo huwa anaumia sana kwani walitoka mbali kimaisha na binti huyo na mpaka sasa haelewi kwanini aliamua kumfanyia hivyo, huku akihoji kwa sababu ya kumpata mpenzi mpya ? au kwanini hakutaka kumueleza ukweli na tukio hilo ambalo lilimfanya akae kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja akijua mtoto wake amefariki dunia, kabla ya kuja kugundua kuwa mtoto huyu yupo hai na mzima wa afya.
Masai Nyotambufu ambaye kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho ya video yake mpya ya muziki unaoitwa "Yero Masai" aliomshirikisha msanii, Richie Mavoko na Kitokolo, video ambayo inayofanywa na kampuni ya Apex videos chini ya Mkurugenzi Pablo kazi ambayo imeanza rasmi leo julai 27 mwenzi huu.
0 comments:
Post a Comment