Basi ndogo (Coaster) likiwa limekwama kupita katika njia ya treni jirani na makao makuu ya stesheni ya ya treni mkoa wa Morogoro kutokana na gari hilo kujaza watu kulikosab
abisha ambapo abiria walilazimika kutelemka ili kupunguza uzito.
Chombo
cha kuhifadhia takangumu kikiwa kimejaa uchafu huku mungine ukiwa
umezagaa chini katika soko la Mawenzi kufuatia halmashauri ya Manispaa
ya Morogoro kushindwa kuondoa uchafu huo kwa wakati na kuleta kero kwa
wateja wanaofika sokoni hapo kupata mahitaji mbalimbali mkoani Morogoro,
Manispaa ya Morogoro ipo katika mpango wa kupandisha hadhi na kuwa jiji
hasa baada ya kupata kichochoe kwa kuibuka nafasi ya tatu katika
shindano la afya na usafi wa mazingira Tanzania bara mwaka 2013.
Askari wa jeshi la polisi wakiwasaidia mafundi kuweka bango katika jengo la kituo kikuu cha polisi mkoa huo ambapo awali kabla ya kuwekwa kwa bango hilo kulikuwa na usumbufu hasa kwa wageni kutambua jengo hilo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali mkoani Morogoro.
Utengenezaji wa tuta ili watu waweze kuvuka eneo stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro mkabara na ofisi ya tiGO makao makuuu mkoani Morogoro.
Safari ya Mikumi kutoka Ruaha katika pori la madaraja 12 wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro
0 comments:
Post a Comment