Muonekano wa eneo la Mnara wa mashujaa uliopo eneo la Posta wakati wa maadhimisho ya sherehe ya kuwakumbuka mashujaa waliopoteza maisha katika vita kuu ya pili ya dunia na zile za Kagera mwaka 1978/1979 iliyoadhimishwa kimkoa eneo hilo la posta mkoani Morogoro leo julai 25/ 2013.
PICHA JUMAMTANDA.BLOG
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera a.k.a Kocha akipokea heshima muda mfupi kabla ya kuanza sher
ehe za kuwakumbuka mashujaa kwa mkoa wa Morogoro.
Bendera akiweka ngao katika mnara wa kumbukumbu wa mashujaa mkoa wa Morogoro.
Hapa akitoa heshima.
Mwanajeshi Mstaafu aliyepigana vita ya
pili ya dunia AC Koplo Hamisi Salum Mlapakolo (94) akiweka zana za kivita za jadi katika mnara wa kumbukumbu wakati wa sherehe hizo.
Haya ndiyo majina ya waliopoteza maisha.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Juma Nondo akiweka mashada ya maua wakati wa uwekaji wa vifaa vya mbalimbali vilivotumika katika vita.
Kiongozi wa gwalide wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa katika hali ya ukakamavu mbele ya kikosi chake.
Kiongozi wa gwalide wa jeshi la magereza akiwa katika hali ya ukakamavu mbele ya kikosi chake.
Kiongozi wa gwalide wa jeshi la polisi akiwa katika hali ya ukakamavu mbele ya kikosi chake.
Mwakilishi wa Shekhe Mkuu wa mkoa wa Morogoro Ustadh Ally Said akiomba dua.
Kiongozi wa dhehebu la Ahamaddiya naye akiwaombea dua njema askari hao waliofariki dunia katika vita wakati wa maadhimisho ya mashujaa.
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoriki jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude akiwaombea dua njema askari waliofariki dunia wakati wa vita katika kilele cha mashujaa.
Kaimu Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi
ya Morogoro, George Pindu akisoma kwa kunukuu moja ya kifungu kwenye kitabu
kitakatifu cha Biblia katika maadhimisho hayo.
Hiki ni kikosi cha maombezi kikitoa heshima zao za mwisho wakati wa kilele cha maadhimisho hayo.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika sherehe hizo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera aliyejishika mikono akiwa na viongozo mbalimbali wakati wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment