BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIGI YA NANE NANE CUP 2013, NNE ZATINGA HATUA YA 16 BORA MTOANO MOROGORO.



MSHAMBULIAJI WA TIMU YA VIJANA YA MORO KIDS U20, GEORGE EMMANUEL AKITAFUTA MBINU YA KUMTOKA MLINZI WA MGULASI SEKONDARI, MICHAEL MWITA MGULASI WAKATI WA LIGI YA NANE NANE CUP 2013 KWENYE UWANJA WA SABASABA MANISPAA YA MOROGORO.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA ya timu nne kati ya tano zimefanikiwa kucheza hatua ya 16 bora mtoano baada ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi ya mtoani ya katika ligi ya Nanenane CUP 2013 yanayoendelea kufanyika uwanja wa Sabasaba mkoani Morogoro.

Timu ya Gereji ndiyo imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora mtoani baada ya kuiondoa mashind
anoni Black People kwa jumla ya bao 1-0, baada ya kuitandika bao 1-0 katika mchezo wa kwanza huku mchezo wa pili wakitoka sare tasa ya 0-0.

Akizungumza na gazeti hili mjini hapa Mratibu wa mashindano hayo ya ligi ya Nanenane Cup 2013, Jumanne Mkali alisema kuwa ligi hiyo imekuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na kila timu kufanya maandalizi ya kutoka huku michezo mitano tayari imefanyika lakini ni timu tatu ndizo zilizofanikiwa kutinga hatua ya 16 bora mtoano.

Mkali alisema kuwa kati ya timu tano zilizochezwa ni timu nne ndizo zimefanikiwa kufuzu hatua ya pili huku timu za Moro Kids na Mgulasi Sekondari zikishindwa kutoa mshindi wa kutinga hatua hiyo ya hatua ya 16 bora mtoani kutoa sare katika michezo miwili ya ligi hiyo ambayo imekuwa na ushindani wa hali ya juu inayotokana na kila timu kusheheni wachezaji wenye vipaji vya mchezo wa soka.

“Hii ligi yetu ya Nanenane Cup 2013 imekuwa na ushindani wa hali juu sana kutokana na kila timu kuwa na vijana wenye vipaji vya soka na zilifanya maandalizi ya kutosha kabla ya kucheza ligi hii”. Alisema Mkali.

Alitaja timu nyingine zilizofuzu hatua ya 16 bora mtoani ni pamoja na Sabasaba United iliyoifunga Welazi FC kwa jumla ya bao 3-1 huku Hiace Terminal ikiiondoa Road Fc kwa jumla ya  bao 4-1. alisema Mkali.

Nyingine ni Chipolopolo iliyoiondoa ya Black Viba baada ya kufungana jumla ya bao 4-4 huku Chipolopolo ikitinga hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini na Sabasaba United ikishinda mbele ya Nato FC kwa jumla ya bao 3-1.

timu za vijana za U20 Moro Kids na Mgulasi sekondari nazo zilishindwa kumpata mbabe katika michezo miwili baada ya kufunga jumla ya bao 2-2.

Baada ya sare hiyo timu hizo ziliamuliwa kumpata mshindi kwa njia ya mikwaju ya penalti ambapo katika mikwaju mitano ya mwanzao Mgulasi na Moro Kids zote zilifanikiwa kupata penalti nne huku kila timu ikipoteza penalti moja na kutoa fursa ya mcheza mmoja mmoja kupiga penalti ambapo kila timu ilipata penalti 10 na mchezo huo kumalizwa kwa sare ya idadi ya bao 12-12.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: