Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea.
Madaktari
wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao ambao wamezaliwa
Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India.
Kwa mujibu wa
taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao imetengana wakati uti wa
mgon
go umeungana na pia wanashare sehemu ya ubavu.
Dr. S.D. Sharma,
wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra sana kutokea hususan
kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama ‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza
kuwa tukio hilo ni la pili kutokea India.
Daktari huyo
aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa
wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa
Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya mapacha hao.
Tatizo kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan mwaka (2011) ambao waliozaliwa wakiwa wameungana vichwa. Watoto hao Rital na Ritag Gaboura walifanikiwa kutenganishwa salama japo kwa tatizo kama lao uwezekano wa kupona hua ni kwa mmoja kati ya million kumi.
Rital na Ritag
Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa
Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa
wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.
0 comments:
Post a Comment