ASKARI WALIOKUFA DARFUR WAKILINDA AMANI HAWA HAPA-MUNGU ZILAZE ROHO ZAO PEMA PEPONI AMINA.
MT 88860 PTE Peter Muhiri Werema 44KJ |
MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ
MT 80581 CPL Mohamed Juma Ally- DFHQ AU
MT 72032 CPL Mohamed Chukilizo 41KJ
MT 87085 PTE Rodney Gido Ndunguru 92 KJ
MT 72121 SGT Shaibu Shehe Othman DFH-AU
MT 75028 CPL Osward Paul Chaula 431 KJ.
DAR ES SALAAM.
RAIS Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
RAIS Jakaya Kikwete ameutaka Umoja wa Mataifa (UN), kuruhusu kutumika kwa mtutu katika operesheni za kulinda amani zinazoendelea.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kutoa heshima zake
kwa wapiganaji saba wa Tanzania waliokuwa Darfur, Sudan katika
operesheni ya kulinda amani ya UN na Afrika (Unamid) ambao waliuawa na
kundi linalodaiwa la wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na
Serikali ya Sudan inayoongozwa na Rais Omar al-Bashir.
Wapiganaji waliouawa ni Oswald Chaula kutoka 42KJ
Chabruma, Songea, Peter Werema (44KJ Mbeya), Fortunatus Msofe (36KJ
Msangani, Pwani), Rodney Ndun
guru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).
guru (92KJ Ngerengere), Mohamed Juma (94KJ Mwenge), Mohamed Chukilizo (41KJ Nachingwea) na Shaibu Othman (MMJ- Upanga).
“Lazima nikiri kuwa taarifa hiyo ya vifo vya
vijana wetu ilinihuzunisha, kunisikitisha na kunikasirisha. Kwa nini
watu wa Darfur wawaue wanajeshi wetu ambao wamekwenda kule kuwasaidia
wapate utulivu ili kunusuru maisha yao, kuwaondolea wasiwasi na
kuwawezesha wafanye shughuli zenye tija kuendesha maisha yao ?.
“Moja kwa moja sikusita kuamini kuwa waliofanya
hivyo ni watu wahalifu. Tangu uhuru ni sera ya nchi yetu kutetea
wanyonge dhidi ya ukoloni, ubaguzi, uonevu, dhuluma na watu wote walioko
katika mazingira hatarishi Afrika na duniani. UN ifanyie marekebisho
sheria ili majeshi yanayolinda amani yawe na nguvu za kujihami ili
kuzuia maafa yanayoweza kujitokeza.”
Hivi karibuni, Msemaji wa Unamid, Chris Cycmanik
alimwambia mwandishi wetu: “Majeshi ya UN mjini Darfur yanaweza kufanya
kazi chini ya Kifungu cha VII ambao inaruhusu kutumia nguvu lakini kwa
hali iliyopo hawafanyi hivyo,” alisema.
Rais Kikwete alisema eneo hilo ni hatarishi kwa
sababu hadi sasa watu 41 kutoka katika nchi mbalimbali wameuawa wakati
wakilinda amani huku wengine 55 wakijeruhiwa tangu mpango wa kulinda
amani ulipoanza mwaka 2007.
“Tumeshawasilisha UN maombi kutaka Kifungu namba
Sita cha kulinda amani kibadilishwe na kitumike Kifungu namba Saba
ambacho kinawataka askari kujihami pindi wanapovamiwa na maadui,”
alisema.
Alisema tayari amewasiliana na Rais al-Bashir
akimtaka kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika
na tukio hilo huku akiwataka wanajeshi kutokata tamaa kwa tukio hilo na
kulichukua kama changamoto katika kujilinda na kuwabaini maadui.
Aliwapa pole wafiwa na kusema Serikali na wananchi
wote wapo pamoja katika kipindi hiki kigumu na kuwataka kuwa na subira.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema kitendo cha waasi kuwaua wanajeshi saba wa Tanzania ni mkakati wa vikundi vya waasi kuhakikisha kuwa jitihada za kuleta amani zinagonga mwamba.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha alisema kitendo cha waasi kuwaua wanajeshi saba wa Tanzania ni mkakati wa vikundi vya waasi kuhakikisha kuwa jitihada za kuleta amani zinagonga mwamba.
Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Jenerali Davis Mwamunyange alisema askari hao pamoja na wengine walikuwa
wakisindikiza msafara wa walinzi wa amani uliokuwa ukitoka katika kambi
yao karibu na Mji wa Nyala.
Alisema walipofika kilometa 25, katika eneo la
Khor Abeche walivamiwa kwa kushtukizwa na kikundi cha watu wachache na
kwa sababu hawakuwa na silaha za kujihami, walishindwa kujitetea na
kusababisha vifo hivyo. MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment