ga Morogoro na Selian Arusha ambazo seherehe hizo zilifanyika kijiji cha Mandela kata ya Magole mwishoni mwa wiki mkoa wa Morogoro.
PICHA NA JUMAMTANDA.BLOG
Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Elias Tarimo akisikiliza risala fupi ya utafiti wa kilimo mseto na mikunde kutoka kwa Mratibu waSemlesa, Bashir Makoko kulia wakati wa sherehe ya sikukuu ya wakulima katika kijiji cha Mandela kuhusu kilimo mseto cha mahindi na mikunde juu ya kilimo hifadhi kupitia mradi wa Simlesa kwa ufadhi wa serikali ya Austaralia na Tanzania ikishirikiana na vituo vya utafiti vya kilimo Ilonga Morogoro na Selian Arusha ambazo seherehe hizo zilifanyika kijiji cha Mandela kata ya Magole mwishoni mwa wiki mkoa wa Morogoro.
Mtafiti kiongozi wa taasisi ya serikali katika mradi wa mifumo ya kilimo endelevu ya mahindi na mikunde mashariki na kusini na kusini mwa Afrika (SIMLESA) nchini,George Iranga kushoto akifafanua jambo kwa mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo wakati
wa sherehe ya sikukuu ya wakulima katika kijiji cha Mandela.
Na Esther Mwimbula,Kilosa.
WAKULIMA wa vijiji vya
Mandela, Magubwige, Mabana, Mfulu, Mdudu viliyopo kata ya magole tarafa ya
magole wilayani kilosa mkoani Morogoro wametakiwa kulima kilimo cha hifadhi cha
mahindi na mbaazi kutokana na zao hilo kuwa na uhakika wa soko ndani na nje ya
nchi.
Mtafiti wambegu za kilimo kutoka
katika kituo cha utafiti cha chollima kilichopo dakawa mkoani humo Geoge Iranga
alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakulima hao na kudai kuwa imefikia
wakati wakulima kulima kilimo ambacho kina manufaa kwao na kinakidhi matakwa ya
wakulima.
Iranga alisema kuwaidadi kubwa
ya wananchi waishio Tanzania wanategemea kilimo kwaajili ya kujikwamua kiuchumi
hivyo wanatakiwa kulima kilimo ambacho kitawaingizia kipato ambacho kitawawezesha
kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuwalipia watoto wao karo za shule.
Aidha pia aliwataka wakulima hao
kushiriki mafunzo mbalimbali ya kilimo cha mseto (SIMLESA)ambayo ambayo imekuwa
ikiwawezesha wakulima kuweza kulima kilimo mseto ambacho kinamanufaa kwa wakulima wadogo ambao wanategemea
kilimo kama msingi wa maisha yao.
Wakizungumza kwa niaba ya
wakulima wenzao Jumanne Bakari na Tatu Hamis walisema kuwa kilimo mseto
kimewanufaisha kiuchumi na kujikwamua na janga la njaa ambalo limekuwa ni kero
wa wakulima wadogo ambao wamekuwa wakitegemea kilimo katika shughuli za
kilasiku.
Hivyo waliwaomba watafiti wa
mbegu na kilimo kufika maeneo ya vijijini kutoa elimu ya kutosha ili waweze
kulima kilimo cha tija na kuachana na kilimo cha mazoea.
0 comments:
Post a Comment