PICHA JUMAMTANDA.BLOG
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akifafanua jambo wakati akiongea na wakulima wa zao la mpunga baada ya mkuu huyo kutembelea maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka na kushoto ni Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka naye akizungumza jambo katika mkutano huo, kutoka kushoto ni, Isaka Mashauri na Mkuu wa mkoa Joel Bendera.
Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kushoto akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa Morogoro Joel Bendera.
Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri akielezea faida ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) mara baada ya Mkuu wa mkoa na viongozi mbalimbali wa serikali kutembelea maonyesho hayo kabla ya kuongea na wakulima.Sehemu ya shamba la mpunga lililopandwa mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
Mkulima wa zao la mpunga, Veronica Urio akizungumza jambo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro (hayupo pichani) juu ya uhaba wa maji wanaopata wakulima katika mashamba ya umwagiliaji wa bonde la Wami-Dakawa yaliyopo wilaya ya Mvomero wakati wa maonyesho hayo.
Viroba vyenye mchele na meza yenye mchele na mpunga kwa ajili ya maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
Sehemu ya wakulima wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka
Afisa Msindikaji na Mtaalamu wa Mapishi Kampuni ya Tanseed International, Skolastica Mashauri (mwenye fulana ya kijani) akipakua chakula kwa wakulima waliodhudria maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5). Kulia ni secretary wa kampuni hiyo, Caroline Chimtembo.
0 comments:
Post a Comment