"...kutumia waandishi wa habari kama vipaza sauti vya serikali;
kukuza, kutia chumvi, kuficha ukweli na hata kusema uongo, ni kudhalilisha
taaluma; ni kutubana na kututanua kama anayechezesha mwanasesere."
Neville,
Hii uliyoandika (Mabadiliko 3 Julai 2013), naipachika hapa chini,
sikubaliani nayo:
Nukuu:
"1.
Udhaifu wa kwanza hata Ikulu ilishindwa kumwandaa Rais kuzungumza na dunia
maswala makubwa ya nchi yetu ambayo tunadhani yangetupa nafasi ya
kutambulika kwamba sisi ni akina nani. Hili lingeweza kufany
ika hata kwa
KUPANDIKIZA maswali ya msingi kwa Waandishi wa Habari wa Tanzania na
kuhakikisha wanapata nafasi ya kuyauliza."
Mwisho wa nukuu.
Hii siitaki. Kutumia waandishi wa habari wa hapa nchini kuuliza maswali
ambayo yatawaonyesha wageni kuwa "sisi ni akina nani?" Neville,
"kupandikiza maswali ya msingi" ili dunia ituelewe sisi ni akina
nani ? Hili, sikubaliani nalo.
Kwanza, kitu gani Marekani haifahamu juu ya Tanzania ? Ubalozi wake uko
hapa na wafanyakazi kibao, wakikusanya taarifa kana kwamba wana vyombo vya
habari. Wanatumia pia wenyeji kutafsiri yaliyoandikwa magazetini na kukalimani
yanayotangazwa redioni na kwenye TV.
Wanakutana na viongozi wakuu na wadogo
serikalini, wafanyabiashara wakubwa, watumishi mbalimbali, viongozi wa asasi za
kijamii, viongozi wa upinzani na wananchi wa kawaida.
Kitu gani hawajui ? Ni
hivi, kwa maana ya taarifa za kawaida na taarifa za kijasusi, Marekani inajua
hata kipele kilichoko kwenye mwili wa rais wetu na sehemu kilipo. Kutumia
waandishi kusema unachotaka, kutafanya waandishi waonekane wa ovyo na wasiojua
kazi zao.
Pili, kutumia waandishi wa habari kama vipaza sauti vya serikali;
kukuza, kutia chumvi, kuficha ukweli na hata kusema uongo, ni kudhalilisha
taaluma; ni kutubana na kututanua kama anayechezesha mwanasesere. Hili
halikubaliki. Kwa hiyo, ikulu (kwa maana ya serikali), itafute njia zake za
kujieleza kwa wageni; ambao "bahati mbaya," wanajua mengi, hata mlo
wetu wa jana.
Tatu, kukosekana kwa waandishi wa habari wengi wa Tanzania kuuliza
maswali, kunaweza kutokana na mambo mawili: Utaratibu uliowekwa wa kuinua
waulizaji; na udhaifu wa waandishi wenyewe. Katika mazingira ya rais wa
Marekani, kunahitajika "ushapu" hata wa kuvunja protokali -
poteleambali! Hawawezi kukukamata.
Najua wakikukamata, watakuachia baadaye.
Hawakujui - itakuwa kashfa ya karne. Unasimama haraka na ghafla na kuweka swali
lako: "Mheshimiwa Kikwete umemwambia Rais Obama kuwa kasi ya kuua raia
imeongezeka na kwamba hivi sasa kazi ya polisi inafanywa na jeshi la wananchi;
ikiwa ina maana kwamba utawala umekushinda?"
Unafahamu ? Rais (mwanasiasa) aweza kujibu kwa njia mbalimbali. Wana
jeuri hawa. Kwa mfano aweza kujibu, "Ehe! swali jingine!" Akakuacha
solemba. Au, "Tumeongea mengi. Hilo utaniuliza baada ya mgeni
kuondoka." Huwezi kuongeza swali kwani "muda hautoshi" na
mwingine atakuwa ameanza kuuliza lake. Unahitajika ujasiri hata wa kuhimili
jeuri ya wakubwa!
Nne, kuuliza katika lugha "mbovu" si hoja sana. Kama swali
lina mantiki, ni mantiki hiyo itakayoliongezea uzito na hadhi mpaka kila mmoja
akaona linastahili kujibiwa. Bali, ili kuondokana na kutoeleweka, hasa katika
mazingira ya kasi kama hayo, siyo vibaya kuandika swali lako, tena kwa ufupi.
Ni vizuri kujua lugha za watu wengine, lakini kutojua kufikia "viwango vya Malikia" - kwani lugha ni utamaduni - kusikufanye ujikunyate na ushindwe kutoa dukuduku lako.
Ni vizuri kujua lugha za watu wengine, lakini kutojua kufikia "viwango vya Malikia" - kwani lugha ni utamaduni - kusikufanye ujikunyate na ushindwe kutoa dukuduku lako.
Hata hivyo, wahusika wanapaswa kuweka wakalimani
ili yeyote aweze kuuliza kwa wepesi, katika lugha yake, huku waliobobea katika
lugha hizo wakiwasilisha kwa lugha ya mlengwa.
Hata kwa upande wa rais, siyo sahihi kulazimisha matumizi ya lugha ya kigeni (Kiingereza) wakati anaelewa vema lugha yake. Hilo nalo liwe funzo.
CHANZO http://ndimara.blogspot.com
Hata kwa upande wa rais, siyo sahihi kulazimisha matumizi ya lugha ya kigeni (Kiingereza) wakati anaelewa vema lugha yake. Hilo nalo liwe funzo.
CHANZO http://ndimara.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment