Harare.
Wazimbabwe leo wanapiga kura kumchagua Rais na wabunge watakaoliongoza taifa hilo kwa miaka mitano ijayo.
Wazimbabwe leo wanapiga kura kumchagua Rais na wabunge watakaoliongoza taifa hilo kwa miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi huo, Rais anayemaliza muda wake,
Robert Mugabe anatetea kiti chake akichuana na mpinzani wake wa siku
nyingi, Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai. Uchaguzi huo unafanyika huku
Mugabe ambaye kupitia chama chake cha Zanu-PF akiwa ametawala kwa miaka
33, akipewa nafasi kubwa ya kumshinda Tsvangirai wa chama cha Movement
for Democratic Change (MDC).
Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kupitia Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc), Bernard Membe alisema ana taarifa
kuwa orodha ya majina ya wap
iga kura haijawekwa wazi tangu juzi, ikiwa ni siku mbili kabla ya uchaguzi wa leo.
iga kura haijawekwa wazi tangu juzi, ikiwa ni siku mbili kabla ya uchaguzi wa leo.
Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, alisema ameshangazwa na hatua hiyo
ya kutowekwa wazi orodha ya wapigakura katika baadhi ya vituo.
Alisema orodha ya wapiga kura siyo nyaraka za siri hivyo zilipaswa kutolewa mapema ili kila mpigakura aone jina lake.
“Orodha inatakiwa itolewe ili watu waione na
kuhakiki majina yao, pia kujua vituo wanavyotakiwa kupigia kura,” Membe
alikaririwa na BBC Focus on Africa akisema.
Tayari MDC kimetishia kwenda mahakamani kutokana
na ucheleweshaji huo unaoweza kutia doa uchaguzi. Katibu Mkuu wa MDC,
Tendai Biti alisema chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya
Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (Zec) ili kupata uhakika wa orodha hiyo.
Uchaguzi wa leo huenda ukamaliza muda wa Serikali ya mseto baina ya
Zanu-PF na MDC.
Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru
mwaka 1980. Alilazimika kuingia kwenye Serikali ya mseto baada ya
Uchaguzi Mkuu wa 2009 kutokana na shinikizo la Sadc ili kumaliza mzozo
wa kisiasa uliokuwapo nchini humo.
Polisi 10,000
Ili kudhibiti usalama katika uchaguzi huo, zaidi
ya polisi 10,000 wamesambazwa kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura.
Redio ya Serikali ilitangaza jana jijini Harare kuwa polisi zaidi
wamepelekwa Jimbo la Midlands wakiwa na silaha kadhaa zikiwamo bunduki
na mabomu ya machozi. Pia ulinzi umeimarishwa katika maeneo ya katikati
ya Harare, Highfield na Mbare.
Wafuasi wa Tsvangirai wameanza kushangilia katika
maeneo ya wilaya mbalimbali hata kabla ya kupiga kura huku wengine
wakiimba kwa kukumbuka ghasia za mwaka 2008, zilizosababisha wafuasi
zaidi ya 200 wa MDC kuuawa. Jino kwa jino. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment