Said Mohamed Saad akiwa hospitaliHAKIKA aliyemmwagia tindikali bilionea Said Mohamed Saad, alifanya kitendo kibaya kupitiliza, kwani athari ambazo amemsababishia ni kubwa kiasi ambacho hata upatikanaji wa tiba mahsusi umekuwa wa kutangatanga.
Taarifa
za ndani na zenye uhakika kuwa Said ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Home Shopping Centre, amekimbizwa Ujerumani kwa matibabu
zaidi baada ya kushindikana Afrika Kusini alikopelekwa awali.
Said
alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa
kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki
la Msasani Mall.
Ilielezwa
kuwa baada ya kumwagiwa tindikali, alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami
Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar es Salaam lakini ndani ya kipindi
kisichozidi dakika 60, alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa
Afrika Kusini.
AFRIKA KUSINI MATUMAINI KIDOGO.
AFRIKA KUSINI MATUMAINI KIDOGO.
Ndugu
wa Said aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa akiwa
Afrika Kusini, ilionekana kwamba bilionea huyo anatakiwa kufanyiwa
oparesheni ya uso ili kuondoa ngozi iliyoathiriwa na tindikali, vilevile
kulifanyia jicho upasuaji.
“Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande wa kulia na mkono wenyewe wa kulia ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu yaliyoathirika zaidi na tindikali,” alisema ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:
“Jicho la kulia lenyewe limepata athari kidogo, kwani inaonekana wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye alifumba macho kwa hiyo tindikali haikuingia ndani ya jicho, iliishia kwa juu.
“Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa wingi juu kwenye jicho la kulia na kutokana na ukali wa tindikali aliyomwagiwa, imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.
“Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani uliafikiwa baada ya kujiridhisha kwamba kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini.
Oparesheni ya uso kubadili ngozi iliyoathirika, vilevile kufanya upasuaji wa jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani.”
AKATAA KUTAJA JINA LA HOSPITALI
Kwa
mujibu wa ndugu huyo, Said aliondolewa Afrika Kusini na kupelekwa
Ujerumani, Agosti 3, mwaka huu na tangu hapo taarifa zake zimefanywa
siri kubwa ili kulinda usalama wake.
“Hata wakati nazungumza na wewe kama mwandishi wa habari, nilijua tu lazima utaniuliza kuhusu jina la hospitali aliyolazwa Ujerumani. Ukweli ni kwamba siwezi kukwambia.
Tunafanya hivyo kwa ajili ya usalama wa ndugu yetu.
“Tukio la kumwagiwa tindikali ni zito sana, imeshajionesha wazi namna ambavyo kuna watu hawampendi, hao maadui wakijua hospitali aliyolazwa, wanaweza kufanya juu chini wamfikie na kumdhuru kwa mara nyingine.
Hilo jambo hatutaki kabisa litokee,” alisema ndugu huyo.
NDUGU, WATOTO WAKE WAZUIWA KWENDA UJERUMANI
Habari zaidi zinabainisha kuwa ndugu wa Said walipanga kwenda Ujerumani kumtembelea lakini walizuiwa kwa sababu awamu hii, viongozi wa familia yake wamezingatia usiri.
“Kuna watoto wake walikwenda Afrika Kusini
na walikuwepo wakati anasafirishwa kwenda Ujerumani lakini waliambiwa
warudi Tanzania kwa sababu kule Ujerumani utaratibu umebadilika.
Watu
wachache wanaohusika na huduma pamoja na usalama wake ndiyo pekee
wanaoruhusiwa,” alisema, akaongeza:“Wapo
ndugu wengine kutoka Saudi Arabia na Oman, vilevile nao wamezuiwa
kwenda Ujerumani kumwona.
Ni katika kuhakikisha mambo hayawi kama
ilivyokuwa Afrika Kusini, maana kule ilishakuwa hatari, ndugu wengine
wanaingia wodini, wanampiga picha na kusambaza mitandaoni. Safari hii
mambo hayo hayatakiwi.”
APELEKWA UJERUMANI BAADA YA JK.
APELEKWA UJERUMANI BAADA YA JK.
Imeelezwa
kwamba Said alipelekwa Ujerumani wiki moja baada ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kwenda kumtembelea alipokuwa
amelazwa kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.Dk. Kikwete,
alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini alipokwenda
kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya
Afrika (SADC), kuhusu pande tatu za umoja huo (Troika of SADC), hivyo
kupata fursa ya kwenda kumjulia hali.
MUNGU AMPONYE SAID.
Dawati
la gazeti hili linamuombea Said apone kwani alionesha moyo wa ukarimu
kwa familia 655 zilizokumbwa na mafuriko eneo la Jangwani, Desemba, 2011
kisha kuhamishiwa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
MTUHUMIWA BADO HAJAKAMATWA
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP
Camillius Wambura alisema kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya
kazi kwa nguvu na umakini mkubwa lakini mpaka sasa halijafanikiwa
kumpata mtuhumiwa.
0 comments:
Post a Comment