Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni akitangaza uteuzi wa makatibu
wakuu na manaibu katika wizara mbalimbali jijini Dar es Salaam jana.
Picha na Venance Nestory.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu wakuu kumi na mmoja na naibu makatibu wakuu 14 wapya katika wizara mbalimbali.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu wakuu kumi na mmoja na naibu makatibu wakuu 14 wapya katika wizara mbalimbali.
Miongoni mwa walioteuliwa ni Katibu Mtendaji wa
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Sifuni Mchome ambaye sasa
anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na aliyekuwa
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deodatus Mtasiwa ambaye anakuwa Naibu
Katibu Mkuu, Tamisemi.
Mtasiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni walisimam
ishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Februari, mwaka jana kupisha uchunguzi dhidi yao, kutokana na kukithiri kwa migomo ya madaktari nchini, pamoja na utendaji wao kulalamikiwa.
ishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Februari, mwaka jana kupisha uchunguzi dhidi yao, kutokana na kukithiri kwa migomo ya madaktari nchini, pamoja na utendaji wao kulalamikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu
Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alisema: “Mtasiwa ameteuliwa kwa kuwa
uchunguzi dhidi yake haujaonyesha kuwa ana kosa lolote, lakini wenzake
(Nyoni) na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David
Jairo bado wanachunguzwa.
Katika uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Peniel Lyimo amehamishiwa Ikulu kusimamia Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN), kuwa Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha
na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo.
Makatibu wakuu walioachwa kwa maelezo kuwa
watapangiwa kazi nyingine ni Sethi Kamuhanda (aliyekuwa Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Kijakazi Mtengwa (Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto) na Omary Chambo (Uchukuzi), huku aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick
Rutabanzibwa akistaafu wa hiari.
Balozi Sefue alisema Rais Kikwete ameanzisha
kitengo kipya katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), kitakachokuwa
kikishughulikia afya ambacho kitasimamiwa na Dk Mtasiwa.
Aidha, aliwataja makatibu wakuu waliohamishwa
wizara kuwa ni Florens Turuka kutoka Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu na Joyce Mapunjo kutoka Viwanda na Biashara
kwenda Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makatibu wakuu wapya
Alisema Jumanne Sagini ambaye alikuwa Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa
wizara hiyo.
Dk Servacius Likwelile ambaye alikuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Dk
Patrick Makungu ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia pia ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa
wizara hiyo.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tamisemi), Alfayo Kidata ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment