BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIOJA CHA MWAKA TANGA !. AMKUNG'UTA MWANAYE, KISHA YEYE MWENYEWE KUPOTEZA FAHAMU.

MWANAMKE mkaazi wa eneo la Sahare jijini Tanga (jina limehifadhiwa) amemtandika mwanae wa kiume hali iliyopelekea wasamalia wema kuingilia zogo holi na kums
hika mama huyu ili asiendelee kumuadhibu mtoto huyo.

Kutokana na kipigo hicho mtoto tayri alishaanza kupoteza sauti baada ya kulia kwa mda mrefu lakini cha kushangaza mama huyu alizirai kwa hasira baada ya wasamalia wema hao mara baada ya kumzuia kabla ya hamu yake ya kumtwanga mwananae haijaisha.

Kwa mujibu wa Mama huyo mara baada ya kuzinduka, wasamalia wema hao waliangua vicheko kutokana na tukio hilo lililovuta hisia kwa wapita njia katika eneo hilo.

Baada ya kuzinduka aliuleza umati wa watu waliomzunguka na kutaja sababu za kumpiga mwanae ni kutokana na kupata malalamiko kutoka kwa jirani yake kwamba mwanae amempiga mtoto wa jirani huyo jambo ambalo lilimchukiza mama huyo.

alisema kuwa adhabu hiyo alichukua ya kumtandika mwanaye ili amfurahishe jirani yake kuwa yeye huyu anamkanya mwanaye pindi anapoletewa mashtaka.chanzo http://www.masainyotambofu.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: