BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Marais wakosa mkutano


Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukifanyika Nairobi, Kenya, umemalizika jana bila kuwepo kwa Rais Jakaya Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwakilishwa na Makamu wake, Dk Mohammed Gharib Bilal, huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikisema Rais Kikwete alishindwa kuhudhuria mkutano huo kwa sababu alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra.
Kukosekana kwa viongozi hao katika mkutano huo kumetafsiriwa kuwa kunatokana na mvutano uliopo sasa kuhusu majeshi ya vikosi vya kulinda amani na waasi wa kikundi cha M23 wanaoipinga Serikali ya Congo.
Waasi hao wanadaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema, “Rais alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand ndiyo maana hakuweza kuhudhuria ila alikuwepo Makamu wa Rais. Hilo la viongozi wa Rwanda na DRC kutokuwepo siwezi kulisemea chochote.”
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi za Maziwa Makuu, walitoa taarifa zao na kujadiliwa.
Share on Google Plus

About Anonymous

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: