BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RWANDA YAICHOKONOA FAMILIA YA RAIS KIKWETE, UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA RWANDA WAZIDI KUDORORA.

RAIS POUL KAGAME RWANDA KUSHOTO NA RAIS JAKAYA KIKWETE KULIA TANZANIA.http://jkikwete.com/js/timthumb.php?src=/photo/gallery/%20big_f4a2e527656fc9736a3a166bfd34194f.jpg&h=337&w=600&q=100MKE WA RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE, MAMA SALMA KIKWETE.

DAR ES SALAAM. 
UHUSIANO kati ya Tanzania na Rwanda unazidi kudorora kutokana vyombo vya habari na baadhi ya maofisa wa nchi hiyo kuanza ‘kuichokonoa familia ya Rais Jakaya Kikwete’.
Tovuti ya News of Rwanda, imedai kuwa mke wa Rais, Salma Kikwete ni ndugu wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana ambaye aliuawa kwen
ye ajali ya ndege wakati akitokea nchini Tanzania mwaka 1993.
Madai hayo yametokana na mtandao wa Wiki Leaks, ambao ulinasa mawasiliano kati ya Ubalozi wa Marekani nchini na Serikali ya nchi hiyo. 

Kadhalika taarifa hiyo ya Wiki Leaks imenukuliwa na magazeti mengine ya Rwanda likiwamo gazeti maarufu la New Times.
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amekanusha taarifa hizo zinazodai kuwa Rais Kikwete ni shemeji yake na Habyarimana.
“Taarifa hizi hazina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Kikwete,” alisema Mwambene.
Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma na si kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Kutokana na tovuti hiyo kuchapisha habari hiyo, wasomaji wake walitoa maoni mengi ya kumkashifu Rais Kikwete.
Baadhi yao walikwenda mbali zaidi kwa kuhusisha habari hiyo na uamuzi wa hivi karibuni wa kuwatimua raia wa Rwanda wanaoishi bila kibali nchini. 
“Kama Mama Salma Kikwete ni binamu wa Habyarimana basi Rais Kikwete amrudishe nyumbani kwao Rwanda,” aliandika msomaji wa gazeti hilo, Osma Kanyambo.
Hali hiyo ni mwendelezo wa vita vya maneno kati ya Tanzania na Rwanda, ambavyo vilianza tangu mwezi uliopita.
Chanzo cha hali hiyo ni ushauri uliotolewa na Rais Kikwete wa kuitaka Rwanda kuzungumza na kundi la waasi la FLDR ambalo limekuwa likiendesha vita kwa miaka 16 sasa wakiwa mafichoni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Rais Kikwete katika hotuba ya mwisho wa mwezi uliopita alikiri kudorora kwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda na kwamba nchi hiyo inamshutumu kutokana na ushauri aliowapa. MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: