BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA BADO WAPO WAPO KWANZA, WATULIZWA NA KOMBAINI YA POLISI.

Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki (kulia) akichuana na mchezaji wa Polisi Kombaini, Magige Machango katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. (Na Mpigapicha Wetu). 
SIMBA jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Kombaini ya Polisi katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba imepata sare hiyo baada ya kutoka kuchezea kichapo kutoka kwa Coastal Union katika mechi nyingine ya kirafiki iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mechi hiyo, Simba ndio ilikuwa ya kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa mshamb
uliaji wake mpya Betram Mombeki.

Mombeki alifunga bao hilo baada ya kuwatoka mabeki wa Polisi ambapo kwa kushirikiana vema na Sino Augustino aliachia shuti na kujaa wavuni.

Katika mechi hiyo, Simba ilicheza bila nyota wake wa kulipwa, hata mchezaji wake nyota Amri Kiemba jana pia hakucheza.

Polisi walisawazisha bao hilo katika dakika ya 57 kupitia kwa Nicholaus Kabipe, bao hilo lilipatikana baada ya washambuliaji wa Polisi kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Simba jana ilimchezesha Abdulhalim Humud, Jonas Mkude na Ramadhani Chombo, kwenye kiungo wakati kwenye safu ya ushambuliaji iliwatumia Mombeki, Agustino, Nasoro Masoud na Issa Rashid na kwenye nafasi ya mlinda mlango alikaa Andrew Ntala ambaye hata hivyo alionekana kuwa na mapungufu mengi kwani mipira ilimponyoka mara kwa mara.

Aidha Simba ilicheza vizuri katika kipindi cha kwanza, lakini hali ilikuwa tofauti katika kipindi cha pili, hasa baada ya kuwatoa Hudud na Chombo ambapo safu ya kiungo ilipwaya na ndipo Polisi walipotumia mwanya huo kupata bao la kusawazisha.

Timu mbalimbali za Ligi Kuu zipo kwenye maandalizi, zikicheza mechi za kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Agosti 24 mwaka huu.

Simba jana iliwakilishwa na: Andrew Ntalla, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Rahim Juma, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Sino Augustino na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.

Polisi FC: Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon Fanuel, Yahya Khatib, Salmin Kiss, Salum Nahoda, Magige Machango, Andrew Bundala, Mokili Lambo, Bantu Admin na Nicolas Kapibe.

Leo kwenye uwanja huo kutakuwa na mechi nyingine ya kirafiki ambapo mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: