BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA WAMTWANGA MWAMUZI BAADA YA KUTANDIKWA BAO NA YANGA SIKUKUU YA EDD EIL FITR MORO.



 
 
Mshabiki wa klabu ya Simba akibonda jiwe ili apate vipande vya mawe kwa ajili ya kufanya vurugua wakati wa mchezo baina ya timu kongwe za Yanga na Simba zilizokutana katika mchezo wa kuwaania mbuzi dume na kuadhimisha sikukuu ya Edd Eil Fitr katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro ambapo mchezo huo ulivun
jika dakika ya 54 baada ya Yanga kupata bao la kuongoza. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 
Mshambuliaji wa timu ya mashabiki wa Yanga Manispaa ya Morogoro, Lutengano Ananisye (Mwaikimba) kulia akishangalia bao pamoja na wachezaji wenzake na shabiki wa timu hiyo dhidi ya mahasimu wao Simba katika uwanja wa Sabasaba Morogoro, mchezo huo haukuweza kumalizika baada ya mashabiki wa Simba kumtandika makofi mshika kibendera namba moja na mchezo huo ambao ulikuwa maalum kwa ajili kusherehekea sikukuu ya Edd Eil Fitr kuvunjika dakika ya 54 wakati Yanga ikiongoza kwa bao 1-0.
Mlinzi wa timu ya mashabiki wa Simba akiondoa hatari katika lango lake huku akizongozwa na mshambuliaji wa timu ya mashabiki wa Yanga Fikiri Hussein (Mmachinga).


Na Juma Mtanda, Morogoro.
PAMBANO la soka la watani wa jadi la mashabiki wa klabu kongwe za Yanga na Simba Manispaa ya Morogoro lilishindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Simba kumkung’ta mshika kipendera namba moja kwa madai ya kukubali bao lililopachikwa wavuni na mshambuliaji wa Yanga, Lutengano Ananisye (Mwaikimba) dakika ya 54 katika mchezo mkali wa kuwania beberu la mbuzi ikiwa ni mchezo maalum wa kusherekea sherehe ya sikukuu ya Edd Eil Fitr na uliofanyika uwanja wa Sabasaba mkoani hapa.

Mshambuliaji wa Yanga, Lutengano Ananisye (Mwaikimba) alifunga bao hilo baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Simba na kushuti la juu na kumshinda mlinda mlango wao na mpira kujaa wavuni dakika 54 kipindi cha pili kufuatia kazi nzuri ya ya kiungo, Hamis Wagala aliyetoa pasi ya bao hilo.

Kuingia kwa bao hilo kuliwachukiza mashabiki wa Simba waliojaa na hasira wakiongozwa na Shukuru Matikila aliyetoka kwenye benchi la ufundi na kumfuata mshika kibendera huyu, Juma Shabaan na kumfokea na kumpiga makofi kabla ya mashabiki wa Yanga kumwokoa na kipigo hicho ambacho mwamuzi wa kati alilazimika kumaliza mchezo huo wakati Yanga wakiongoza kwa bao 1-0.

Hasira hizo za mashabiki wa Simba zilitokana na kukataliwa kwa bao lililofungwa na, Boniface Mapunda dakika ya tatu kipindi cha kwanza aliyefunga kwa njia ya adhabu ndogo nje ya mstari wa 18 ambapo mpira huo ulipigwa moja kwa moja na kujaa wavuni huku mwamuzi wa mchezo huo, Raphael Ikambi akiwa tayari ametoa ishara kwa kumtaka mpigaji kupiga pigo ndogo.

Mratibu wa mchezo huo, Athmani Mswagati alisema kuwa baada ya kuvunjika kwa pambano hilo ambalo mshindi alitarajiwa kukabidhiwa zawadi mbuzi mnyama mwenye thamani ya Sh60,000 na kuwa mchezo huo utarudiwa siku nyingine.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: