BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TINDIKALI SHAMBULIO LINALOTISHIA UHAI WA VIONGOZI NA WATU MAARUFU TANZANIA.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeLqQbz4k9LzJs6qBpYpidOjynO3ffDlKh2TznvmU_tZE_OJSaqgSGTipwPMIPYr0jVm-yv_KbPJpaqL8eIey-Y3ddwdB-wdcJ1QjfZkYBaQi5KYqd3yHE4Mn0VolB1U6Xgwq-elcswbo/s640/........................sheikh+tindikali.jpgKaimu Sheikhe wa wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha Saidi Mak
amba. https://encrypted-tbn3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcRqAvSJaGtolK14NSQEZWQPw097w2-XeIbBsdIVpTwPX3hious5kushoto Katie Gee  kabla ya kumwagiwa tindikali huko Zanzibar na kulia  baada ya kumwagiwa tindikali.http://1.bp.blogspot.com/-ZsGljS1yiWY/UfFm6J0afwI/AAAAAAAAj-w/ieNOJTOYUl0/s320/shopping+centre.jpgMfanyabiashara maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center(HSC), Said Mohamed Saad, ameliwa kwa kumwagiwa tindikali.Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga.

Chande Abdallah na Hans Mloli
LICHA ya serikali kutangaza kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kimiminika hicho bado kinapatikana kirahisi mitaani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele walitoa tamko la kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali ambao umesababisha kujeruhiwa kwa watu wengi nchini.


Jumatatu iliyopita, mapaparazi wetu walizama mitaani na kuanza kuisaka bidhaa hiyo ili kuona kama upatikanaji wake una ugumu wowote.

Katika maabara moja iliyopo Kinondoni, Dar mapaparazi waliambiwa tindikali inapatikana, nusu lita shilingi 45,000. Maabara moja iliyopo Ilala, bidhaa hiyo inapatikana kwa nusu lita shilingi 30,000, lakini bei inaweza kupungua hadi shilingi 25,000.


Mapaparazi hawakuishia hapo, walifika hadi Kipawa jijini Dar ambapo walikutana na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ambaye alisema anaiuza bidhaa hiyo kwa shilingi 16,000 tu na hashushi zaidi ya hapo. Tindikali hiyo ni mali ya shule.

Huku akirekodiwa video kwa siri (ipo Global), mwalimu huyo alisema amekuwa akiwauzia watu mbalimbali bidhaa hiyo na alikiri kwamba huwa hawaulizi wanakwenda kufanyia nini kama ambavyo hakuwauliza mapaparazi wetu.


Hadi mapaparazi wetu wanaondoka shuleni hapo, mwalimu huyo hakujua kama wanunuzi waliokwenda kununua tindikali hiyo ni ‘wapelelezi’ mahiri kutoka Global Publishers.

Mitaani watu wanasema tindikali ni silaha mpya ya maangamizi kwa kizazi cha sasa ambapo kila kukicha hofu ya watu kujeruhiwa na kimiminika hicho inazidi kupanda.


Mpaka sasa, Watanzania wengi wameshamwagiwa tindikali na watu wanaosadikiwa ni wabaya wao. Miongoni mwa watu waliokumbwa na balaa hilo ni mmiliki wa Home Shopping Center, Said Mohamed Saad, Shehe wa Bakwata wilayani Arumeru, Issa Makamba na mtu  aliyedaiwa ni mpiga debe wa CCM, Igunga  Mussa  Tesha.

Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Katibu wa Mufti Zanzibar, Shehe Fadhili Soraga na wasichana wawili raia wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: