BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIBAKA KARIAKOO WACHACHAMAA, WATANZANIA KUWENI MAKINI WAKATI WA MAANDALIZI YA SIKUKUU

_DSC1648_DSC1671_DSC1677Maskini binti wa watu kapata kovu bila sababu ya msingi, enyi vibaka shauri yenu, siku zenu zakaribia
_DSC1680     Harakati za kujiandaa na sikukuu ya Eid. Kama unavyojua watu kariakoo huongezeka zaidi na vibaka nao hutumia mwanya huo waubize wa watu kutafuta mahitaji yao.
     Binti mmoja aliyekuwa katika pilikapilika za maandalizi ya sikukuu ya Eid Kariakoo alikutwa na mkasa baada ya kibaka mmoja kutaka kumpora begi lake la mkononi.
Binti huyo hakuwa tayari kuachia begi lake kirahisi, kitendo ambaacho kilimuudhi kibaka huyo na kumpelekea kumkata na kisu kiganjani binti huyo na kumtishia asipige kelele kwa kuwa atamfanyia kitu mbaya.
   
   Kwa ujasiri aliokuwa kuwa nao binti huyo alipiga kelele zilizopelekea wasamaria wema katika eneo hilo kumsaidia na kumtia nguvuni kibaka huyo eneo la Kariakoo kituo cha mabasi yaendayo Mbagala.
  
   Hatimaye Polisi jamii wakisaidiana na Maaskari wa Usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumtia nguvuni kibaka huyo.
 
Picha na Juma Omari.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: